Bondia Hassan Mwakinyo akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye pambano lake dhidi ya Bondia Arnel Tinampay raia wa Ufilipino litakalofanyika Novemba 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa. 
Promota Jay Msangi, anayeratibu pambano hilo akizungumzia maandalizi na kuwataka wadau wa michezo kujitokeza na kuweza kudhamini, na pambano hilo litatanguliwa na mapambano matano ya utangulizi kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi.(Kushoto) Bondia Hassan Mwakinyo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BONDIA Mtanzania mwenye rekodi ya kushinda mapambano 17 na kupoteza moja Hassan Mwakinyo  atapanda ulingoni Novemba 29 katika pambano la Vitasa Fight Night dhidi ya Arnel Tinampay raia wa Ufilipino kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mwakinyo mwenye rekodi ya kushinda kwa KO mapambano 15, na kupoteza Mmoja dhidi ya Mtanzania Shaban Kaoneka amekuja na kauli mbiu ya do or die  (kufa ua kupona).

Mwakinyo amesema anafahamu kama mchezo huo ni mgumu hususani kulingana na ubora wa mpinzani wake ambaye kwa nchini Ufilipino ana rekodi nzuri na katika mapambano aliyoyapoteza hajawahi kupigwa KO.

" Siwezj kumdharau mpinzani wangu ndio maana naendelea na mazoezi chini ya Kocha wangu, nafahamu ni bondia mzuri, mgumu na mzoefu na hana rekodi ya kupigwa Knock Out (KO), ni mgumu na anahitaji mbinu za ziada na mazoezi ili kumpiga," amesema Mwakinyo.

"Pambano hilo ni la raundi 10, katika uzani wa Super Welter"

Mwakinyo amesema, anajipanga kuweza kushinda pambano hilo, atatumia mbinu zake kuhakikisha anabakiza heshima nchini kwani anapambana kwa ajili ya Taifa na kuliwekea heshima.

"Nitacheza kufa ua kupona kuhakikisha naendeleza rekodi yangu, natambua ugumu wa pambano hili na ubora wa mpinzani wangu ambaye ni bondia huyo ambaye ni namba moja katika viwango vya ubora nchini Ufilipino kwenye uzani wa super welter," amesema.

Promota wa pambano hilo, Jay Msangi amesema Mwakinyo na Tinampay watasindikizwa na mapambano matano ya utangulizi ya mabondia kutoka nchini na nje ya nchi ambao tayari tupo kwenye mazungumzo nao.

Msangi amesema, wapo na mazungumzo na IBF,WBO kuangalia kama pambano hili litakuwa la ubingwa na kama sio basi mshindi acheze pambano la ubingwa.

" Thamani ya Mwakinyo ni zaidi ya milion 100, ila tayari maandalizi yanaenda vizuri na tunazidi kuwaomba wadau wa mchezo wa ngumi kuja kudhamini pambano hili ambapo tayari tumeshapata baadahi ha wadau na pambano hili litarushwa na katika nchi mbalimbali duniani,"amesema Msangi.

Wadau wa michezo hususani wa ngumi wameombwa kujitokeza kwa wingi kwenye pambano hilo, na ushindi wa Mwakinyo utawavutia wacheza ngumu wakubwa duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...