Na Said Mwishehe,Arusha-Michuzi TV
JUKWAA la Utawala wa Mtandao kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAIGF) wamekutana jijini Arusha kwa lengo la kujadili kwa pamoja ukuaji wa matumizi ya mtandao kwa maendeleo ya jamii ya nchi hizo.
Kupitia mkutano huo wawakilishi na wadau wa nchi hizo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda,Rwanda ,Burundi na Sudani Kusini wametumia nafasi hiyo kujadili kwa kina kuhusu matumizi sahihi ya mitandao katika kuleta maendeleo huku kila nchi ikilezea namna inavyotumia mtandao.
Akizungumza katika kongamano hilo Mwakilishi kutoka Burundi Joel Nkurunzinza amesema kutokana na kukua kwa teknolojia kumeifanya Dunia kuwa kijiji hivyo EAIGF zimeona ni vema kutumia jukwaa la majadiliano ili kuwaelimishana na kubadilishana uzoefu.
"Lengo la nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuhakikisha tunakwenda pamoja katika eneo hili la matumizi ya mtandao,"amesema na kuongeza matumizi hayo yaende sambamba na kuheshimu sheria zilizopo kwa kila nchi.
Ameongeza kuwa kupitia kongamano hilo, kuna mambo mengi ya kujifunza na yatatoa muelekeo sahihi kuhusu namna bora ya kutumia mitandao. "
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Rwanda Grace Ingabine ambaye ni Mkurugenzi wa RICTA amesema amefurahishwa na majadiliano ya kongamano la EAIGF huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa nchi yao imepiga hatua kwani asilimia 96 ya wananchi wa mjini na vijijini wanatumia mtandao.
"Kwetu wadau wa mtandao tumekuwa tukikutana kujadili kuhusu teknoloji ya mawasiliano kila ifikapo Novemba, lakini kupitia kongamano hili la EAIGF tumeamua na sisi tutakuwa tukikutana la nchi kwetu kila ifikapo Juni na hiyo itatoa nafasi ya kushiriki katika kongamano la EAIGF ambalo linafanyika Oktoba,"amesema.
Mwakilishi wa Tanzania wa EAIGF Nazar Nicholas amesema kwa upande wa Tanzania kumekuwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kuhakikisha mitandao inatumika kwa usahihi na baadhi ya hatua ambazo zimechukuliwa ni pamoja na kuwepo kwa sheria ya mtandao .
Wakati huo huo Getrude Mweta kutoka Chama cha Viziwi Tanzania ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa EAIGF kuhakikisha watu wenye ulemavu wanakuwa na mazingira rafiki ya kushirikishwa katika majadiliano yanayoyaandaa.
Amesema watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali wamekuwa wakishirikishwa katika makongamano lakini changamoto kubwa inayowakutana ni kukosekana kwa mawasiliano ya majadiliano"Hapa leo tunao viziwi , watu wenye matatizo ya uono na walemavu wa viungo na wanahitaji kujua kinachoendelea lakini changamoto ni nani anawasaidia kuwafikishia ujumbe."
Mwakilishi wa EAIGF kutoka nchini Kenya Barrack Otieno amesema nchini kwao wanaendelea na kupiga hatua katika matuminzi ya mitandao na kwamba kongamano hilo limesaidia kuwapa nafasi ya kujua kipi ambacho wanatakiwa kukiboresha.

Wadau wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAGF) wakiwa katika kongamano la majadiliano kuhusu matumizi ya mtandao
Wawakilishi wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAGF) kutoka nchi za Tanzania,Kenya,Burundi,Rwanda,Sudan Kusini na Uganda wakiwa meza kuu wakati wa majadiliano hayo wakiendelea leo Oktoba 17,mwaka 2019 jijini Arusha
Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia majadiliano wakati majadiliano hayo
Mmoja wa wakalimani akitoa ufafanuzi kwa watu wenye ulemavu waliohudhuria kongamano la majadiliano ya mtandao ambayo yameandaliwa na Jukwaa la Utawala wa Mtandao kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAGF)
Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo akitoa maoni yake wakati wa majadiliano hayo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...