
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Dominic Dhanah akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bomba Weekend katika kituo cha kuuza mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Paytech LTD, Sameer Hirji, akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya BombaWeekend kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Dominic Dhanah.

Baadhi ya wateja wakikaribishwa na wafanyakazi wa Puma Energy kwa ajili ya kujaza mafuta kwa kutumia kadi ya Master Card kwenye kituo cha kuuza mafuta cha Puma Energy Upanga.

Bw. Modestus Chambu mmoja wa wateja wa kampuni ya Puma Energy akijaziwa mafuta kwa kadi ya Master Card kwenye kituo cha kuuza mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es salaam.

Wateja wakiendelea kuhudumiwa na wafanyakazi wa Puma Energy Upanga jijini Dar es salaam.

Bw. Modestus Chambu mmoja wa wateja wa kampuni ya Puma Energy akiwaelezea waandishi wa habari faida anazozipata kwa kujaza mafuta kutumia mfumo wa Kielektroniki Master Card.
KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania, Selcom Paytech LTD na Mastercard kwa wamezindua kampeni ya pamoja iitwayo BombaWeekend yenye lengo la kurejeshea asilimia tano ya fedha watakayotumia watakapojaza mafuta katika vituo vya Puma Energy endapo watalipia kupitia Mastercard QR.
Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar s Salaam na itaendeshwa kwa wiki 11, kila Ijumaa hadi Jumapili kuanzia saa 10 hadi 12 jioni kupitia mtandao wa Puma wenye vituo 52 nchi nzima. Pamoja na dhumuni la kuzawadia watumiaji wa huduma hiyo, Bomba Weekends ina dhamira ya kuchangia katika juhudi za serikali za kurasimisha malipo na kuhamasisha uchumi wa malipo ya kieletroniki ili kufikia malengo ujumuishaji wa kifedha wa nchini Tanzania.
Pia imeelezwa kwamba mchakato mzima wa kurudishia pesa wakati wa Bomba Weekends unaendeshwa kupitia huduma ya zawadi kwa wateja ya Qwikrewards iliyoundwa na Selcom Paytech LTD mahususi kwa watumiaji wa Mastercard QR.
Na kwamba Qwikrewards inamuwezesha mtu yeyote kukusanya pointi au kupata pesa taslim kupitia akaunti iliyounganishwa na namba yake ya simu kila afanyapo malipo kutumia Mastercard QR. Watumiaji Qwikrewards wanaweza kukomboa pointi walizokusanya kwa kupiga 150*15 na kuzitumia katika maeneo zaidi ya 30,000 nchini ambapo Mastercard QR inakubalika kama njia ya malipo.
Aidha Mastercard QR imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake nchini mwaka 2018 hadi sasa kupelekea kukubalika na watoa huduma mbali mbali zaidi ya 30,000 kuwa na uwezo wa kupokea malipo kutoka mitandao yote 7 ya simu na benki 15 nchini.
Akizungumza kwa kina kuhusu kampeni hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah amesema "Bomba Weekends inahamasisha wateja we kulipia mafuta katika vituo vyao kwa kutumia njia rahisi, haraka na salama zaidi na kunufaika papo hapo kupitia Qwikrewards kutoka Puma.
Amesema ushirikiano huu unadhahiri kwamba Puma ni kiongozi wa katika sekta ya mafuta inapofikia kujiunga na suluhisho bunifu za malipo ambazo hurahisisha malipo kwa wateja wetu na kutuwezesha kutoa huduma bora zaidi katika vitu vyetu."
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Paytech LTD, Nd. Sameer Hirji, alionyesha matumaini makubwa kuelekea uchumi wa malipo ya kielektroniki akisisitiza kuwa ni lazima taasisi ambazo zinaongoza mchakato huo kuongeza thamani kwa wateja ili kuwapa hamasa zaidi kutumia malipo ya elektroniki.
"Kupitia Bomba Weekends tukishirikaina Puma Energy pamoja na Mastercard QR tumedhamiria kuwazawadia wateja watakaolipa kielektroniki katika matumizi yao ya kila siku, mafuta yakiwa sehemu kubwa ya matumizi hayo.
" Tunaamini kwamba tunavyozidi kurahisisha na kuimarisha upatikanaji na upokeaji wa malipo ya kieletroniki ndivyo tutazidi kuwajengea Watanzania imani ya kutoka nyumbani bila pesa taslim. Tukiwa na Qwikreward na maeneo zaidi ya 30,000 ambapo Mastercard QR inakubali kitaifa tunaamini tunaongoza mabadiliko kuelekea malipo ya kielektroniki na malengo ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania,”amesema .
Wakati huo huo wadau mbalimbali wanatumia mfumo wa malipo kwa njia ya kieletroniki wamesema wamefurahishwa na uamuzi wa kampuni hizo kuungana kuhakikisha wanahamasisha ulipaji wa fedha kwa njia hiyo ambayo ni salama na yenye kurahisisha malipo.
Wamesema katika kipindi hiki cha kampeni hiyo wataitumia vema ili kupata asilimia tano ambayo imetolewa kama sehemu ya kupata fedha ambayo Puma wameamua kuirejesha kwa Watanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...