Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Kepteni saidi Hamadi mmoja wa Marubani walioleta ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner kuoka Seattle Marekani alipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo kwenye viti vya marubani wa Boeing 787-8 Dreamliner alipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Mke wa Rais Mama janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakifurahia jambo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuipokea ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ndani ya Boeing 787-8 Dreamliner alipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuaga baada ya kuongoza mamia ya wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine na wadau akikata utepe kuashiria kupokewa kwa ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo wakisiliza maelezo toka kwa Kepteni Dennis Mshana mmoja wa Marubani walioileta ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Seattle Marekani hadi katika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama alipoongoza wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na marubani na wanaanga waliokuja na ndege wakati alipoongoza mamia ya wananchi katika mapokezi ya ndege hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini alipoongoza mamia ya wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wa Taasisi Mbalimbali za Umma na Binafsi alipoongoza wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Mzee Omary Mkali, mmoja wa wazee waliofika katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26
Oktoba, 2019 ameungana na wananchi wa Dar es Salaam kuipokea ndege mpya aina ya
Boeing 787-8 Dreamliner
iliyonunuliwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha usafiri wa anga na kukuza
uchumi hapa nchini.
Mapokezi
ya ndege hiyo yamefanyika jengo namba moja (Terminal
One)
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Spika
wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi,
Mawaziri na Naibu Mawaziri, Mabalozi wa Nchi mbalimbali, Wabunge, Makatibu
Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.
Ally Hapi, viongozi wa Dini, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa taasisi
mbalimbali na wafanyabiashara.
Akizungumza
na wananchi mara baada ya kutua kwa ndege hiyo kutoka Seattle nchini Marekani
ilikotengenezwa, Mhe. Rais Magufuli ameelezea furaha yake ya kufanikiwa kwa
mpango wa kuimarisha usafiri wa anga baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kununua
ndege 11 kwa ajili ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambapo 7
zimeshawasili na zingine 4 zitawasili kwa vipindi tofauti hadi kufikia June
2020.
Mhe.
Rais Magufuli amesema Watanzania wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa
kuwa ndege hizo zimenunuliwa kwa fedha zinazotokana na kodi zao na hivyo ametoa
wito kwa kila Mtanzania kuendelea kuchapa kazi na kulipa kodi ili Serikali
iweze kufanya mambo mengi zaidi ya kuwaletea maendeleo.
“Kwa hiyo
fedha zenu zinajulikana hadi kule Marekani kwamba Watanzania wanaweza kununua
kitu kizito kama hiki, hongereni sana Watanzania, siku zote mtembee kifua mbele
ndugu zangu Watanzania, mnaweza, Watanzania tunaweza na Waafrika tunaweza,
hakuna kinachoshindikana.
Kikubwa
kinachohitajika ni matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana kutoka kwa wananchi,
hongereni Watanzania, kwangu mimi najisikia raha sana, ninajisikia raha kuwa
kiongozi wa Tanzania, lakini najisikia raha zaidi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi, kwa sababu haya yamezungumzwa kwenye Ilani ya Uchaguzi.
We mi ndege
kama hii inashuka hapa? kwa sababu ni lazima tujiulize kwa nini hayakushuka zamani?
Huo ndio ukweli bila kuficha, kwa nini mi dege hii isubiri Magufuli awepo ndio
ishuke” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Amemshukuru
Rais wa Marekani, Mhe. Donald Trump kwa kutambua juhudi za Tanzania katika
maendeleo na kununua ndege kutoka Marekani kwa ajili ya kuimarisha huduma za
usafiri wa anga.
Balozi
wa Marekani hapa nchini Dr. Inmi Patterson ameipongeza Tanzania kwa kuboresha
usafiri wa anga na ameelezea juhudi hizo kuwa zitaboresha uchumi na zitavutia
uwekezaji.
Mhe.
Rais Magufuli ameipongeza menejimenti na wafanyakazi wa ATCL kwa kazi
wanazofanya ikiwemo kuingiza mapato ya kiasi cha dola za Marekani Milioni 14 (sawa na shilingi na shilingi Bilioni 31 na Milion
892)
na amewataka kuzitunza ndege hizo vizuri na kuhakikisha Shirika linaendeshwa
kwa ufanisi.
Ndege
hiyo mpya ina uwezo wa kubeba abiria 262 na kusafiri saa 18 bila kutua, Mhe.
Rais Magufuli ameshuhudia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiikabidhi
kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dr. Leonard Chamriho ili itumike kwa ATCL.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amekubali ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Makonda
la kupatiwa shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya ya
Ubungo Jijini Dar es Salaam na amemuagiza Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo kutafuta fedha hizo ili ujenzi uanze.
“Hatuwezi
kuwaacha wananchi wa Ubungo wateseke, wakitaka kutibiwa mpaka waende Wilaya za
jirani, hapana, tutajenga Hospitali ya Wilaya ya Ubungo, Ubungo hoyeee” amesisitiza
Mhe. Rais Magufuli.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar
es Salaam
26
Oktoba, 2019
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...