
Msanii wa Bongofleva Roma akiwajibika jukwaani wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana Jijini Arusha.

Msanii wa Bongofleva Mario akiwajibika jukwaani wakati akitumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana Jijini Arusha.

Roma na Stamina Wasanii wanaounda kundi la Rostam wakitumbuiza katika jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta SIZe Yako liliofanyika jana Jijini Arusha

Msanii Rosaree akitumbuIza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo Arusha

Msanii wa bongoflava Jux akiwa jukwaani katika tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia leo jijini Arusha.

Msanii wa bongoflava DogoJanja akinogesha wimbo na Roma jukwaani katika tamasha la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia Leo Arusha.
NA Ally Mvungi, Arusha
TAMASHA la Muziki, Msimu wa Tigo Fiesta2019 jana liliwafurahisha wana chugga kwa kishindo jijini Arusha huku Rostam likifunika kwa kuwapagawisha washabiki luluki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Mbali na wasanii hao kukonga vilivyo nyoyo za washabiki wa muziki wa kizazi kipya wasanii wengine walikuwa Rosa Ree, Juma Jux,Ruby, Country boy,Fid Q,Weusi.
Washabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid walishindwa kujizuia kutokana na makamuzi ya nguvu yaliyowaacha hoi yaliyofanywa na kundi la Rostam, na huku Dongo janja akijiunga nao kufanya makamuzi ya kipekee.
Tamasha hilo limefanyika Arusha lilikuwa na mvuto na msisimko mkubwa ambapo mashabiki kutoka viunga vya jiji hilo la kitalii walisuuzika nyoyo na mara kadhaa walishiriki kuimba nyimbo za wasanii mbalimbali hasa kundi la Rostam.
Akizindua tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema waandaaji wa Tigo Fiesta 2019 kwa ubunifu na uamuzi wao wa kuzindua tamasha hilo hawakukosea ikizingatiwa jiji hilo ni kitovu cha utalii kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati.
“Arusha ni kisima cha burudani kutoka na kuwa na wapenzi wengi wa muziki wa kizazi kipya hivyo niwapongeze Clouds na Tigo kwa ubunifu wao wa kuandaa na kuzindua tamasha lao hapa.Sisi kama mkoa tutaendelea kuwaunga mkono.Pia tamasha hili mbali na kutoa burudani lina umuhimu kiuchumi, linatoa ajira za muda mfupi,linaongeza kipato cha wananchi wetu na waandaaji nao wananufaika,”alisema Gambo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba, kampuni hiyo ya mawasiliano itaendelea kushirikiana na kuiunga mkono Clouds ili kuhakikisha wanawapatia Watanzania burudani yenye vionjo na ladha tofauti tofauti.
Tamasha hilo sasa linaelekea mjini Tanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...