Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
BONDE la Wami/ Ruvu limesema kuwa baada ya Waziri wa Maji kutangaza tozo za visima vya majumbani kumefanya baadhi ya wafanyabiashara wa Hoteli na Vituo vya Mafuta wametumia fursa hiyo ya Waziri wa Maji kutolipa tozo za visima ambapo Bonde hilo linatarajia kuwafikisha mahakamani kwa kukiuka ulipaji wa tozo wa visima.
Hata hivyo bonde la Wami/Ruvu linashangazwa baadhi ya wafanyabiashara wenye hoteli na vituo vya mafuta walikubali kulipa tozo za visima vya maji kidogo kidogo lakini baada ya Waziri wa Maji kutangaza kuondoa tozo za visima vya maji ya majumbani wafanyabiashara hao wametumia mwanya huo wa kutolipa tozo hizo.
Akizungumza na waandishi wa haari jijini Dar es Salaam Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani amesema kuwa bonde limeweka mkakati kwa wote kuwapeleka mahakamani na waliokuwa wanalipa kidogo kidogo nao watalipia mahakamani huko.
Mhandisi Ngonyani amesema kuwa watu wasipolipa tozo vyanzo vya maji hiaviwezi kuendelea kutokana baadhi ya watu kufanya ukaidi wa kulipa tozo ambazo ziko kwa mujibu wa sheria.
‘’Hawa tutapewapeleka mahakamani nasubiri mwanasheria afanye upembuzi wa wadaiwa kutokana na tozo hizo ndizo zinafanya bonde liendelee kulinda vyanzo vya maji sasa tutawezaje kupanda miti katika vyanzo hivyo wakati watu wanakaidi kwa makusudi kulipa tozo ambazo zimewekwa kisheria’’amesema Mhnadisi Ngonyani.
Amesema kuwa serikali inataka kuchimba bwawa la maji kwa ajili ya dharula pale inapotokea vyanzo vya maji vimekuwa havina maji basi bwawa hilo lifanye kazi ya kupeleka katika mitambo na kazi hiyo ya uchimbaji inatokana na tozo za watu mbalimbali.
Aidha amesema kuwa katazo la ulipaji wa tozo za visima vya majumbani hakufanyi sasa uchimbaji wa visima kwenda bila tozo hili halikubariki watu wote wanaotaka visima lazima wapate kibali pamoja na kulipa tozo na maji yatakayopatikana lazima yalipiwe tozo kwa ajili ya maabara ya kufanya uchunguzi wa maji hayo.
Baadhi ya wadaiwa Wafanyabiashara ya Vituo vya Mafuta hawa hapa TSN Oil (T)LTD ,Simba Oil ,World Oil,OKOD International, Kobil.Mantrack pamoja na Gapco na Baadhi Wafanyabiashara wa Wamiliki wa Hoteli hizi hapa Dar Live ,Ice Land Hotel, Grand Villa.
Tozo kwa wadaiwa hao ni zaidi ya milioni 328 huku wakiwa wamepata tozo hizo ni sh.milioni 149 tu huku Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) ikiwa haina deni ambapo Bonde limeipongza Dawasa.
Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza na waandishi haari kuhusiana na wadaiwa tozo za maji katika bonde hilo hatua watazozichukua kutokana na kukaidi ulipaji wa tozo ,jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...