Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako amesema kuwa Serikali imeendelea kuwajengea walimu uwezo katika maeneo ya kazi ikiwa ni pamoja na kuimarisha maeneo ya kujifunzia na kuhakikisha shule zinakuwa na vifaa vya kutosha.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa shule za msingi na sekondari katika Mikoa yote 31 nchini na Mikoa 5 ya Tanzania bara Profesa. Ndalichako amesema kuwa anathamini sana mchango wa TEHAMA kwa kuwa sayansi na teknolojia kwa sasa vimekuwa chachu ya maendeleo hivyo ubunifu kwa sasa ni lazima utiliwe mkazo zaidi.

" Kwa washiriki 1029 waliopata mafunzo haya katika vituo vya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Chuo kikuu cha Dodoma na Chuo cha Teknolojia Mbeya wakawe mabalozi kwa walimu katika maeneo yao ya kazi na Serikali imeanza kuwekeza katika vifaa na walimu na wakawe chachu kwa wanafunzi ili somo hilo liwe la lazima mashuleni kutokana na umuhimu wake" ameeleza Prof. Ndalichako.

Aidha amewapongeza Taasisi ya Mawasiliano kwa Wote kwa kushirikiana na ofisi ya TAMISEMI na Wizara ya Elimu wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu katika kuhakikisha walimu kutoka maeneo mbalimbali wanapata mafunzo hayo.

Pia ameishukuru Serikali ya India kupitia ubalozi wake nchini kwa kujenga kituo cha umahiri cha TEHAMA katika taasisi ya teknolojia (DIT) na katika Chuo cha Nelson Mandela jijini Arusha na kuwataka wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali ili kuwezesha mafunzo kwa walimu laki moja na themanini kote nchini.

Awali akizunguza kuhusu mafunzo hayo Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Profesa. Preksedia Ndomba amesema; huu ni mwaka wa 62 tangu taasisi hiyo ianzishwe na wamekuwa wakitoa wataalamu na mafunzo kwa viongozi wa taasisi mbalimbali wakiwemo maafisa wa jeshi.

Prof. Ndomba amesema kuwa baada ya kutolewa kwa mafunzo hayo ambayo yamehitimishwa kwa mtihani wa upimaji matokeo yatatumwa Wizara ya Elimu na Ofisi ya TAMISEMI ambako walipendekeza walimu hao kushiriki mafunzo hayo.

Pia mwakilishi wa walimu 534 katika kituo cha Taasisi ya Teknolojia (DIT) Mwalimu. Anzawe Chaula amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa wamejifunza mada tano ambazo wanaamini zitawasaidia katika taasisi zao wanazofanyia kazi.

" Tumepata ziada ya chaki, tumejifunza kutumia vifaa vya TEHAMA pamoja na kuvifanyia marekebisho pindi vinavyoharibika tunaiomba Serikali itafute wadau zaidi ili tuweze kupata vifaa vya TEHAMA" ameeleza.

Ameeleza kuwa uelewa mdogo waliokuwa nao awali kuhusiana na TEHAMA umepata mbinu mpya ambapo amesema mahusiano bora baina ya shule za Msingi, Sekondari na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) yatazidi kuleta tija zaidi katik sekta hiyo adhimu ya Elimu.





Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na walimu wa shule ya msingi pamoja na washule za sekondali jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari yaliyokuwa yakifanyika jijini Dar es Salaam katika vituo tofauti tofauti.
 Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha umahiri wa TEHAMA, (ITCOEICT), Daudi Mboma akizungumza na walimu wa shule ya msingi na sekondari jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari yaliyokuwa yakifanyika jijini Dar es Salaam katika vituo tofauti tofauti.
  Balozi India nchini Tanzania, Sanjiv Kohli akizungumza na waalimu wanafunzi wakati wa kufunga mafunzo yaliyokuwa yakitolewa jijini Dar es Salaam katika vituo mbalimbali,wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari.
Mwalimu Wanzawe Chaula, akisoma Risala wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari yaliyokuwa yakifanyika jijini Dar es Salaam katika vituo tofauti tofauti mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako. Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)Profesa Preksedia Marco akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Tehama kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari yaliyokuwa yakifanyika jijini Dar es Salaam katika vituo tofauti tofauti.
  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, (DIT)Profesa Apollinaria Pereka akizungumza na walimu wa shule za sekondari na shule za msingi jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufunga mafunzo yaliyokuwa yakitolewa jijini Dar es Salaam. 


 
Baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule za msingi wakipokea vyeti
vya kufunzu kumaliza mafunzo ya TEHAMA wakati wa kufunga mafunzo yaliyokuwa yakitolewa jijini Dar es Salaam katika vituo mbalimbali.


Baadhi ya walimu wa shule za Msingi pamoja na shule za Sekondari walihudhulia mafunzo ya TEHAMA wakiwa katika mkutano wa ufungaji mafunzo hayo jijini Dar es Salaam leo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...