Na Woinde Shizza globu jamii,Arusha
Unywaji wa maziwa ya ng'ombe ambayo hayajapimwa na mtaalamu husababisha magonjwa mbalimbali kwa binadamu ikiwemo ugonjwa wa kifua kikuu pamoja na brusela.
Hayo yameelezwa na daktari wa mifugo ambaye pia ni mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha Grande Demam ,Dr Deo Temba wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo alibainisha kuwa wakati huu kumekuwa na wananchi wengi wanaokubwa na magonjwa haya ,huku wengi wao ukiwachunguza unakutwa magonjwa yao yametokana na unywaji wa maziwa
Alibainisha kuwa ipo haja ya serikali kuunda sheria itakayo muamrisha mwananchi kununua maziwa yaliopimwa na yale ambayo yamepita kiwandani ili kuweza kusaidia kupunguza tatizo hili
"kumekuwepo na wananchi wafugaji ambao sio waaminifu unakuta kabisa anajua ng'ombe wangu ni mgonjwa au nimempa dawa sitakiwa kukamua na kwenda kuuza lakini kwavile anauroho wa fedha anakamua na kwenda kuuza na akifika kwa mnunuzi ananunua na kutumia bila kujua"alisema Temba
Alibainisha kuwa maziwa ambayo yanapita viwandani hupimwa kwanza kabla ya kuingizwa kiwandani,huku akifafafanua kuwa hupimwa kama yamewekwa maji au kama mnyama huyo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wowote naikibainika ni mazuri ndipo harakati zingine hufanyika
"kuna wananchi ambao wanachukuwa maziwa uko mtaani hayaja chekiwa ubora ,hayajapimwa lakini pia wakifika majumbani kwao hawayachemshi kama inavyotakiwa wanachemsha kwa muda mchache hivyo iwapo maziwa yale au ng'omb e yule alikuwa na magonjwa vile vijidudu vilivyopo kwenye maziwa havifi na ndio vinasababisha magonjwa haya yanayotoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu"alifafanuaTemba
Aidha alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wanakunywa maziwa ambayo hayanaubora kwani asilimia kubwa ya wauzaji wa maziwa haya wamekuwa wanayaweka maji kitu ambacho kinasababisha maana halisi ya maziwa haya kupotea na ubora wake pia kuisha kabisa kutokana na maji wanayoyaweka huku wengine wakiwa wanajaza maji nakuchanganya vitu vingine kama unga wa ngano ili maziwa yao yaonekane mazito
Alimalizia kwakuwataka wananchi kuacha kutumia maziwa yanauzwa kiolela badala yake watumie maziwa yaliotoka viwandani kwani yamechemshwa vizuri ,yameangaliwa kama yanaubora,pia Baada ya kuletwa nawateja yameangaliwa kama mnyama huyo anamagonjwa au kama alikuwa anatumia madawa.
Kwaupande wa mwananchi aliejitambulisha kwa jina la Japheti Mwahakila alisema kuwa nikweli wao kama wananchi wamekuwa wananunua maziwa kiholela bilakujua kama ng'ombe huyo ni mzima au la kitu ambacho kinawafanya baadhi yao kupata magonjwa mbalimbali yawanyama.
Aliomba serikali kupitia mamlaka ya chakula na dawa kutoa elimu zaidi kwa wafugaji juu ya mazara yanayoweza kutokea iwapo atauza maziwa ambayo mnyama wake ni mgonjwa ili kuweza kuwasaidia wananchi kwani anaamini wakipewa elimu ya kutosha tatizo hili litamalizika kabisa.
Picha ikionyesha meneja masoko wa kiwanda cha Grande Demam Japheti Mwahakila akionyesha namna kampuni hiyo inavyosindika siagi kabla ya kwenda kwa mteja(picha na Woinde Shizza ,Arusha)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...