Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi,Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, amewataka wamiliki wa maeneo ya kazi kuzingatia usalama na Afya mahali pa kazi kwa Wafanyakazi wao.
Akizungumza katika hafla ya kufunga Mafunzo maalumu ya Usalama na Afya mahali pa Kazi kwa wakaguzi wa OSHA yaliyofanyika jijini Arusha, Mhe. 
Mhagama amesema kila ajira zinapozalishwa zinaenda sambamba na ajali pamoja na magonjwa, amesema hivyo waajiri wanapaswa kuhakikisha wanazingatia usalama wa wafanyakazi wao, amesema  kukua kwa haraka kwa teknolojia inayotumika viwanda na maeneo mengine ya kazi kunagusa moja kwa moja afya na usalama wa wafanyakazi. 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda amesema, walishirikiana na Shirika la Kimataifa la Workplace Health Without Borders (WHWB) katika mafunzo hayo kwa Wakaguzi, Khadija amesema Shirika hilo linalofanya kazi nchi mbalimbali dunia ikiwemo Tanzania  pia limejenga uwezo kwa wakaguzi  wa OSHA kuhusu masuala ya usalama na Afya, hivyo kupelekea na mabadiliko ya Teknolojia, amesema Shirika hiloa limetoa msaada wa vifaa mbalimbali ambavyo vitatumika kwaajili ya kufanya kaguzi mbalimbali meeno ya kazi.
Nao Washiriki wa Mafunzo hayo kutoka OSHA, wamesema elimu waliyoipata wataitumia kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi, hususan kaguzi mbalimbali watakazokuwa wanazifanya.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akiwa na kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi Khadija Mwenda kwenye Kufunga Mafunzo Kwa Wakaguzi wa OSHA jijini Arusha.

Mkaguzi wa Afya ya Mazingira kutoka OSHA, Bi Glory Boniventure akimuelezea Mhe. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, matumizi ya Vifaa ambavyo vimetolewa na Shirika la Kimataifa la Workplace, Health Without, Borders (WHWB) vitakavyotumiwa na Wakaguzi


 Mhandisi  Maria Ndaskoy akimuelezeaWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama vifaa vya Umeme vilivyotolewa na WHWB kwa OSHA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...