Na Felix Mwagara, MOHA, Dodoma.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.
Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Lugola, jijini Dodoma, leo, ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia. 
Waziri Lugola alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini. 
“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.
Kwa upande wake Balozi Sanbe, alimshukuru Waziri Lugola kwa mazungumzo waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Ethiopia na Tanzania.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe, masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Nchi ya Ethiopia na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dodoma, leo. 
 Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kulia), akimfafanulia jambo Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (kushoto), wakati walipotembelewa na Balozi wa Ethiopia Nchini, Yonas Yosef Sanbe, Ofisi za Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimuaga Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe, baada ya kumaliza mazungumzo yao, Ofisini kwake, jijini Dodoma, leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima. 
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kulia) akimuaga Balozi wa Ethiopia nchini, Yonas Yosef Sanbe, baada ya Balozi huyo kumaliza mazungumzo na Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (hayupo pichani), jijini Dodoma, leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ethiopia Nchini, Yonas Yosef Sanbe, baada ya Balozi huyo kuwatembelea viongozi hao, jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...