Waziri wa Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama, akizungumza na maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)juzi mkoani Simiyu alipotembelea banda la shirika hilo kwenye kilele cha maonesho ya tatu ya mifuko ya uwezeshaji program na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi. Picha na mpiga picha wetu.
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetakiwa kushirikiana na Shirika la kuendeleza viwanda vidogo (SIDO) ili wajasiriamali kupata maeneo bora ya kuzalishia katika karakana za SIDO
Waziri wa Sera,Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama ametoa wito huo jana mkoani Simiyu alipotembelea banda la TBS wakati wa kilele cha maonesho ya tatu ya mifuko ya uwezeshaji program na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Mhagama alitoa wito huo kufuatia maelezo kutoka kwa ofisa wa shirika hilo, Roida Andusamile kuwa wajasiriamali wengi wanashindwa kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozizalisha kutokana na kutokuwa na majengo bora ya kuzalishia.
Akizungumza na washiriki wa maonesho hayo, Mhagama ameitaka mifuko inayotoa mikopo kwa wajasiriamali kuongeza kasi ya utoaji wa mikopo hiyo ili iweze kufikia wajasiriamali wengi nchini.
“TBS mnapaswa kushirikiana na SIDO ili kuwawezesha wajasiriamali kuzalishia katika kalakana za SIDO na hatimaye waweze kuzalisha kwa kuzingatia viwango na kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo," alisisitiza Mhagama.
Naye mtenndaji Mkuu wa Baraza hilo, Beng'I Issa amewataka wananchi wa Simiyu kuchangamkia fursa zilizotolewa katika maonesho haya kwani uwepo wa maonesho haya utaibua chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Simiyu.
Mhagama alisema utoaji huo wa mikopo uwe na riba nafuu ili wajasiriamali wengi wanufaike nayo na amelitaka Baraza la Uwezeshaji kusimamia mifuko ya uwezeshaji kuendelea kujitambulisha na kujitangaza kwa wananchi kupitia programu mbalimbali.
Katika maonesho hayo TBS ilipata fursa ya kuwatembelea wajasiriamali wapatao 60 wanaozalisha bidhaa mbalimbali na kuwapatia utaratibu ili waweze kusajili majengo wanayozalishia , bidhaa na kuthibitisha ubora wake.
Alisema maonesho haya pia yanakutanisha wajasiriamali na taasisi za serikali lengo likiwa ni kuwawezesha kurasimisha biashara zao na kuhamasisha matumizi ya mifuko ya ya kijamii pamoja na mtandao kwa wajasiriamali.
Maonesho haya yaliyoanza Oktoba 14,2019 mpaka Oktoba 20 2019 mbali na wajasiriamali yameshirikisha taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi zipatazo 48.
Pia wananchi waliotembelea banda la shirika hilo walielimishwa umuhimu kwa kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora na TBS na kuangalia muda wa matumizi wa bidhaa wanazozinunua badala ya kuangalia bei.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...