WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumapili, Oktoba
20, 2019) kwenda Urusi
kuhudhuria mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika
na Urusi (Russia-Africa Summit), utakaofanyika jijini Sochi, Urusi, Oktoba 23 –
24, 2019.
Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya
Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.
Mkutano huo
utakaoendeshwa chini ya uenyekiti wa pamoja (Co-chaired) wa Rais wa Shirikisho
la Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), unalenga kurejesha na kuimarisha uhusiano
baina ya mataifa ya Afrika na Urusi ambao uliyumba baada ya kusambaratika kwa “Union
of Soviet Socialist Republic” (USSR) mwaka 1991.
Mkutano huo
wa Wakuu wa Nchi na Serikali utafanyika katika sehemu mbili, ambazo ni
Kongamano la Biashara (Russia Business Forum) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 23,
na Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Urusi na Afrika uliopangwa kufanyika Oktoba
24, 2019.
Waziri Mkuu atashiriki
kwenye mikutano yote miwili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...