Na Editha Edward, Michzi TV, Tabora 

Msanii mahiri wa bongo fleva Ally Salehe Kiba Maarufu kama Alikiba ameshiriki mbio za Tabora green marathon kwa kukimbia km 2.5 zilizoanzia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora hadi viwanja vya Ali Hassan Mwinyi zilizofanyika hii leo mkoani humo 

Akizungumza katika mbio hizo msanii alikiba amesema mbio zimemfanya achangamshe mwili na akili kwani michezo zinajenga urafiki pia zinakutanisha watu na zinaimarisha mwili hivyo amefurahi kushiriki pamoja na mkuu wa mkoa huo na amewahimiza wananchi wa mkoa huo kuwa na utamaduni wa kukimbia ma kufanya mazoezi ili waweze kuwa imara kimwili.

 Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri naye alikuwa ni miongoni mwa wakimbia mbio hizo ambapo yeye amekimbia mbio umbali wa km2.5 ambapo amesema msanii alikiba ni mfano wa kuigwa kwani tangu afike mkoani humo katika tamasha lake la muziki linalojulikana kama unfogetabletour ameweza kufanya mambo mengi ya kijamii ‘’Msanii.

Pichani ni Msanii Wa bongo fleva Alikiba na mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakikimbia mbio za Tabora Green Marathon 
Pichani ni Msanii Wa bongo fleva Alikiba na mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakikimbia mbio za Tabora Green Marathon 
Pichani ni Msanii Alikiba akimvalisha medani mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kukimbia mbio za km 2.5
Msanii Alikiba akipanda mti nje ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi baada ya kukimbia mbio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...