Meneja wa mauzo ya rejareja wa Azania Bank Limited, Jackson Lohay  (katikati) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuwatangaza washindi wa promosheni ya Amsha Ndoto iliyoendeshwa na benki hiyo kwa lengo la kuwahamasisha wateja wake kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba.


Benki ya Azania (ABL) leo imewatangaza washindi wa awamu ya tatu na ya mwisho wa promosheni yake ya ‘Amsha Ndoto’ ambayo ina lengo la kuwahamasisha wateja wake na umma wa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba itakayowasaidia kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.

Promosheni hii ambayo ni ya mizezi mitatu ilianza rasmi tarehe 27/06/2019 na ilifika tamati tarehe 27/09/2019 huku ikihusisha wateja wa Azania Benki wa zamani na wale wapya na ilijikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti pamoja na Watoto Akaunti.

Mwezi Agosti, droo ya kwanza ya promosheni hii ilifanyika ambapo jumla ya washindi watatu walipatikana ambao wote kwa pamoja walijishindia jumla ya shilingi millioni 8. Vivyo hivyo, droo iliyofuata ilifanyika mwezi Septemba ambapo pia washindi watatu walipatikana wakijishindia jumla ya kiasi cha shilingi milioni 8.

Akitangaza washindi kwenye droo ya tatu na ya mwisho ambayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Jackson Lohay, amesema benki imetimiza ahadi ya kuwapatia zawadi washindi walioshoriki kwenye promosheni na kwamba zawadi wanazopewa zinawasaidia kutimiza ndoto zao. “Katika droo mbili zilizopita tulipata washindi kutoka Amaeneo mbalimbali ya nchi yetu ya Tanzaniana wote walipewa zawadi zao kama walivyostahili, kwa ujumla washidni wote sita waliweza kujishindia kiasi cha shilingi milioni 16,” amesema Lohay.

Kwa mujibu wa Lohay, washindi wa droo ya mwisho ya promosheni hii ambao wamepatikana baada ya droo kufanyika ni; (kiasi cha fedha walichojishindia kwenye mabano);

1. Frank Godfrey Nyange (Tsh2.2m)
2. Anna Said Lyimo (Tsh 3m)
3. Venancy Benny Loshia (Tsh 3m)

Akitoa pongezi kwa washindi wa promosheni, Lohay amewahasa wateja wa ABL kuendelea na utamaduni wa kujiwekea akiba kwani kwa kufanya hivyo wanakuwa wanajihakikishia kuwa na fedha za kutosha kwenye akaunti zao kwa ajili ya matumizi yao ya siku za usoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...