Mkuu wa Kitengo cha
Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo (katikati)
akipokea cheti kutoka kwa Mjumbe wa
kamati ya maandalizi ya Mshindano ya Gofu ya Hisani yaliyoandaliwa na Klabu ya
Rotari ya Bahari, Hemaly Jethwa kwa kutambua udhamini wa benki hiyo katika
mshindani hayo yaliyofanyika katika Viwanja cha gofu vya Gymkhana jijini Dar es
Salaam hivi karibuni yakiwa na lengo la kukusanya fedha kusaidia wenye mahitaji
maaalumu ikiwa ni pamoja na mradi wa kusaidia upatikanaji wa maji safi na
salama, vyoo na kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao katika Shule ya Sekondari
Mtakuja iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam. . Kushoto ni Meneja Mahusiano wa
NBC, Joseph Lema. Mashindano hayo yaliwashirikisha zaidi ya wacheza gofu 104.
Picha mbalimbali za tukio la mashindano
ya gofu ya hisani yaliyoandaliwa na Klabu ya Rotari ya Bahari na kudhaminiwa na
Benki ya NBC. Mashindano hayo
yalikuwa na lengo la kukusanya fedha na kusaidia wenye mahitaji maaalumu katika
jamii ikiwa ni pamoja na mradi wa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama,
vyoo na kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao katika Shule ya Sekondari Mtakuja
iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yaliwashirikiosha zaidi
ya wacheza gofu 104.
Picha mbalimbali za tukio la mashindano
ya gofu ya hisani yaliyoandaliwa na Klabu ya Rotari ya Bahari na kudhaminiwa na
Benki ya NBC. Mashindano hayo
yalikuwa na lengo la kukusanya fedha na kusaidia wenye mahitaji maaalumu katika
jamii ikiwa ni pamoja na mradi wa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama,
vyoo na kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao katika Shule ya Sekondari Mtakuja
iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yaliwashirikiosha zaidi
ya wacheza gofu 104.
Maofisa wa Benki ya Taifa ya Biashara
(NBC), wakipiga picha ambapo pamoja na kutoka huduma za maji na kofia kwa
wakimbiaji, washiriki pia walipata nafasi ya kujulishwa huduma mbalimbali za
kibenki zitolewazo na benki hiyo.
KATIKA kuendeleza jitihada zake za kurudisha
sehemu ya faida yake kwa jamii, Benki ya NBC imedhamini hafla maalumu ya kuchangisha
fedha iliyoandaliwa na Klabu ya Rotari ya Bahari jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Hafla hiyo iliandaliwa na klabu hiyo ili
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wenye mahitaji maalumu katika jamii ya
watanzania ikiwemo mradi wa kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo
na ujenzi wa kituo cha kufundishia kwa njia ya mtandao katika Shule ya
Sekondari ya Mtakuja iliyopo eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam
jana, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa NBC, Evance Luhimbo
alisema NBC kwa miaka kadhaa imekuwa ikishughulisha katika kusaidia shughuli za
jamii katika maeneo mbalimbali kama vile
elimu, afya na masuala ya ujasiriamali,
“Sisi ni jukumu letu kama benki kurudisha katika
jamii sehemu ya faida tuipotayo katika biashara yetu, NBC ni benki kongwe yenye
uzoefu katika kutoa huduma bora za kibenki kwa zaidi ya miaka 52, hivyo
tutaendelea kusapoti miradi kama hii yenye kuleta tija katika jamii”, alisema.
Pamoja na hayo alisema mara baada ya kupokea
maombi ya kuchangia hafla hiyo kutoka Klabu ya Rotari, benki yao haikusita kuitikia
wito kwani ni imani jamii ikiwezeshwa kiuchumi na kielimu na jamii ikiwa na
afya bora inaweza kuchangia vizuri katika kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Aidha Bwana Lhimbo aliitaja baadhi ya shughuli
za kujamii ambayo NBC imefaya ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule za mkoani
Lindi, Zanzibar, msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa Morogoro pamoja
na kutoa elimu ya masuala ya kifedha na ujasiriamali katika shule mbalimbali
nchini.
Baadhi ya miradi ambayo imeshafanikishwa na
Klabu ya Rotari ya Bahari ni pamoja na matibabu ya moyo kwa watoto katika
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ukarabati wa maktaba katika shule ya
msingi buyuni, upanuzi wa kituo cha mafunzo ya ufundi stadi katika kituo cha
masista cha Carmel, Kurasini, ukarabati wa maktaba katika Shule ya Sekondari ya
Mtakuja pamoja na kutoa misaada ya aina
tofauti katika vituo vingine vya walemavu na wasiojiweza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...