Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam


Mwanamuziki Zahir Alli Zorro, wakati akiwa katika bendi ya JKT Kimulimuli, alipata kuimba wimbo akimsifia mwanamke mrembo wa Misri Cleopatra.

Baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza sifa zote hizo alizozipamba nguli huyu zikoje?

Cleopatra ni nani?

Cleopatra alikuwa Malkia maarufu zaidi kati ya wote waliowahi kutawala nchi ya Misri.

Alizaliwa katika mji wa Alexandria mwaka wa 69 K.K (Kabla ya Kristo), wakati wa utawala wa familia ya Ptolemy kwenda kwa Ptolemy XII.

Cleopatra lilitokea kuwa jina maarufu ndani ya familia, kwani mama yake alilipenda kiasi cha kuchukiza kwa wengine lakini pia ndiye alikua binti mkubwa .

Cleopatra hakua Mmisri, ispokuwa asili yake alikuwa mMacedonia, familia yake ikitoka katika kipindi cha utawala wa Alexander The Great.

Cleopatra alikuwa mtawala wa kwanza katika familia yake ambaye aliongea lugha halisi ya Misri.



Urithi wa utawala wa Ptolemy

Mfalme wa Misri, Ptolemy wa XII, wakati anafariki mnamo mwaka wa 51 K.K. akaacha utawala kwa kijana wake mdogo mwenye miaka 12 Ptolemy XIII. 

Lakini aliagiza kwamba, kijana huyo atawale pamoja na dada yake mkubwa, Cleopatra. Pia ni lazima amuoe, kama desturi ya utawala wa ukoo wa Ptolemy, ingawa ndoa hiyo ilikua ni kama kuigiza.

Ukizingatia umri wa mumewe huyo, Cleopatra alitawala yeye binafsi kama atakavyo.Cleopatra aliyekuwa na umri wa miaka 18, mapema alithibitisha umahiri na uwezo mkuu wa kutawala, hususan katika historia ya kipindi hicho cha Medditerania.

Lakini ukaribu wake na utawala wa Roma, baadae unakuja kupoteza uhuru wa Misri.

Caesar na Cleopatra: 48-44 K.K

Kuwasili kwa Julius Caesar Alexandria, kulimpa fursa Cleopatra kuonekana Ulimwenguni, kwa wakati huo.

Aliiachia Misri mikononi mwa Julius Caesar ambaye baada ya kushinda vita Pompey akawa mtawala mwenye nguvu katika dola ya Roma.

Julius Caesar aliamua kupumzika kati ya 47 – 7 K.K huko Misri, akimsaidia Malkia huyo Cleopatra hata kuangamiza majeshi ya kaka yake (ambaye hakuweza kufua dafu).

Mara baada ya Caesar kuondoka Alexandria, Cleopatra anajifungua katika majira ya Kiangazi mnamo mwaka wa 47 K.K, akadai kuwa mtoto ni wa Caesar, na pia anafanana sana na baba yake huyo.

Katika mwaka wa 46 K.K Caesar alimualika Cleopatra Roma pamoja na mwanae (ambae mara baada ya kuzaliwa alipachikwa jina Caesarion, “Caesar mdogo). Walikaribishwa katika jumba la kifahari likiwa na kila aina ya anasa. baadae Caesar aliuawa.

Baada ya Caesar kuuawa mwaka wa 44, Cleopatra aliamua kurudi Misri na mwanae.

Antonius na Cleopatra, 41- 31 k.k

Misri ya Cleopatra bado ulikuwa ni utawala ambao ni huru. Lakini karibu kila sehemu ya ukanda wa Mediterranean unajihusisha na siasa za Roma, kuna uvumi ulienea Roma kwamba Cleopatra alimsaidia “Cassius, mmoja kati ya waliomuua Caesar.

Katika majira ya kipupwe mnamo mwaka wa 41, Marcus Antonius aliamuru majeshi ya Roma kwenda upande wa Mashariki, na kuamuru Cleopatra aje aeleze juu ya tuhuma dhidi yake katika makao makuu yake huko Anatolia.

Cleopatra alivuka Medditerania kwenda kumuona Marcus Antonius, lakini akiwa katika hali ya ujeuri, tena akiwa hana msimanzi.

Alisafiri hadi kambi ya Antonius iko Tarsus, maili kadhaa kwenda mto Cydnus. Malkia aliwasili akiwa katika Boti ya kifahari, akiwa amevaa mavazi ya kuvutia ya mahaba, yenye asili ya Kigiriki.

Hazuiliki kutamanika na mapenzi yake mara yanaangukia ndani ya nyumba ya Jenerali Marcus Antonius.


Cleopatra alimualika Antonius amtembelee Alexandria.

Antonius alikubali mwaliko wake kwenda Misri kumtembelea. Alipowasili Alexandria wakati muafaka kwa ajili ya kupumzika wakati wa majira ya baridi.

Baada ya Antonius kuondoka kurudi Roma, Cleopatra patra anajifungua mapacha, mvulana na msichana.Wanakaa muda mrefu, hadi mwaka wa 37 K.K ndipo Cleopatra na wanawe wanaungana tena na Antonius.

Antonius Alimuagiza Cleopatra kwenda Antioch, Syria ambako huko alimuoa.Sasa wakajionesha waziwazi pamoja, wakaungana kumpinga Octavian, mpinzani mkubwa wa Antonius katika Roma.

Jenerali Antonius akiwa na jeshi lenye nguvu eneo la Mashariki , akawa na uwezo wa kumpa mkewe huyo mapokezi makubwa ya ndoa zaidi ya yale yaliokuwa Mashariki ya Kati (Syria).

Katika desturi ya tawala nyingi za Mashariki, Cleopatra na Antonius sasa wakawa na uwezo wa kuabudu katika miungu mmoja.

Katika Ugiriki wanakua “Dionysus (Antonius) na Aphrodite (Cleopatra), katika desturi za Wamisri wanakua Osiris na Isis, hali kadhalika.

Mkutano katika Alexandria 44 K.K

Watu wengi wanakusanyika kwa ajili ya mkutano katika Alexandria, macho yao yakiangalia yanayojili toka kwa utawala huo.

Katika jukwaa kuu aliketi Antonius na mkewe Cleopatra, akiwa amevaa mavazi ya sherehe maalum mithiri ya Mungu wa kike wa Misri.

Katika viti vingine vinne vya kifalme walikuwa wameketi watoto wao wote watatu, pamoja na ‘Caesar –mdogo’, mtoto mkubwa wa Cleopatra, kwa Julius Caesar.

Mnamo majira ya jioni katika tafrija hiyo, ambayo baadae ilijulikana kama “harambee katika Alexandria”, Antonius aliugawa utawala wa Mediterranean Mashariki kwa familia yake hiyo mpya.

Antonius alimtangaza Cleopatra kuwa “Malkia wa Wafalme, na “Caesar-mdogo kuwa Mfalme wa Wafalme, kwa pamoja wakitawala Misri na Cyprus wakati huohuo tawala zingine aikatawaliwa na watoto wao. Kwa Alexander, kijana wake mkubwa (umri miaka 6), aliwapa sehemu ya Mashariki mwa Euphratia, kwa Mapacha, dada zake Alexander, Cleopatra, aliwapa Libya na Tunisia, na kwa kijana wake mdogo, Ptolemy Philadelphus (miaka 2) ambae alivaa mavazi ya kihistoria ya Macedonia, anamgawia Syria na sehemu kubwa ya Anatolia.

Ikawa sherehe inayovutia, lakini ambayo baadae italeta uhasama na vita.

Actium na baadaye: 31-30 K.K

Mapigano kati ya majeshi ya Octavianus na yale ya Antonius na Cleopatra yanafanyika Actium, Ugiriki katika mwezi September. Pande zote mbili, wana majeshi makubwa ya miguu na yale ya farasi, lakini pia swala jingine ni meli za kivita za Roma, waliokuwa nazo pia.

Antonius na Cleopatra wanafaida ya kuwa na meli 500, 100 zaidi ya zile za Octavianus ambazo ni 400. Hizi ni zana za mbao ambazo ni imara sana. Zikiongozwa na na jeshi mahiri linalofikia askari hadi ya 250. Antonius anapanga jeshi lake la meli, pamoja na Cleopatra na majeshi yake nyuma, hazina kubwa ya Misri, tayari kwa mapigano.

Chanzo halisi cha mapigano haya hakijulikani. Lakini Octaviunus ameenda kinyume na matakwa ya wenza hawa wa utawala wa Mashariki.

Katika mapigano ya Actium meli za Octavianus zilishinda;

Katika hatua flani, Antonius anamjulisha Cleopatra juu ya meli zake , na mpango wakuvunja mapigano na kutoroka nae.

Antonius na Cleopatra wanafanikiwa kurudi, katika milki ya Cleopatra. Lakini wote wanaamua kujinyonga katika mwaka unaofuata, wakati Octavianus alipowasili Misri na jeshi lake. Marcus Antonius anaamua kujiua, malkia alijaribu kumshawishi kutofanya hivyo, lakini ilishindikana. Alielewa ya kwamba angepelekwa Roma na kuoneshwa kama mfungwa mbele ya halaiki. Hapa aliamua kufa tar. 12 Agosti 30 KK.


“ASP” Nyoka aliemuua Cleopatra 30 K.K

Cleopatra aliamua kujiua , kama ishara ya ushujaa mkubwa. Mara nyingi alichukulia ‘serious’ uwajibikaji wake kwa Misri.

Pia ndiyo mtawala pekee wa kutoka ukoo wake aliyejifunza na kujua kuongea lugha ya Misri.

Malikia alitambua kama akiwa hai tayari atakua mfungwa wa Octavianus.

Akilindwa na askari wake wachache katika sehemu ndogo ya makazi yake, aliagiza sumu ndogo ya nyoka, ASP, ambayo iliingizwa kwa siri kupitia kwenye kikapu chake anachotumia kuletewa matunda.

Cleopatra alivaa mavazi yake mazuri ya ki-Malikia, akalala katika kiti chake cha dhahabu. Akamu kujitoa kafara kwa “Amen-Re” Mungu wa Jua wa Misri.


Anakufa kwa sumu ya nyoka huyu (ASP).

Muda wa mwisho wa uhai wa Malkia ulikuwa kama ‘maigizo’, na unakumbukwa sana katika historia ya maisha yake. Na pia unaweka kikomo cha utawala wa Ptolemy katika Misri.

Octavianus alimtafuta pia Caesarion kwa sababu aliogopa mtoto wa Caesar angekuwa hatari kwake, akamuua. Akawachukua watoto wote watatu wa Marcus Antonius, akawaonesha mbele ya halaiki ya Roma kuonesha ushindi wake.

Pia aliichukua Misri kuwa sehemu ya utawala wa Roma, na kuchukua milki zote za ufalme wa Misri.Huyo ndiye Cleopatra aliyewababaisha baadhi ya watu nyakati hizo.

Mwisho.

Makala hii imeandaliwa kwa msaada mkubwa wa mitandao.

Mwandaaji anaptikana kwa Namba: 0784331200, 0736331200, 0767331200 na 0713331200.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...