Msanii wa Bongomuvie, Yusuf Mlela akizungumza na waandishi wahabari wakati akitambulisha kazi yake mpya ya tamthilia ya Kauli aliyomshirikisha Hemed Suleiman maarufu kama Hemed PHD na wengine wengi itakayorushwa kwenye mtandao wa kuuza na kununua kazi za sanaa wa Swahiliflix
Msanii wa Bongomovie Hemed Suleiman maarufu kama hemed PHD  akizungumza na waandishi wahabari wakati wa kitambulisha kazi mpya ya tamthilia ya Kauli ya Yusuf Mlela itakayorushwa kwenye mtandao wa kuuza na kununua kazi za sanaa wa Swahiliflix.

        Na Khadija seif, Michuzi TV
MSANII wa Bongomovie Yusuf Mlela awahimiza wasanii kubadilisha soko la filamu kwa kutengeneza filamu zenye maudhui yanayogusa jamii zaidi.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa utambulisho wa tamthilia yake mpya "Kauli" ambayo wasanii kama hemed phd na wengine wengi wameshiriki katika tamthilia hiyo.

Hata hivyo amesema tamthilia hiyo itakua ikipatikana kwenye mtandao wa kuuza na kununua kazi za filamu wa Swahiliflix.

"Kutokana na teknolojia kukua kwa kasi zaidi kwa sasa hata wadau wa sekta hii ya filamu wameamua kuleta vitu vya tofauti zaidi ili kufanya kazi za sanaa kuendelea kuishi na kupatikana kwa urahisi zaidi na ndio maana Swahiliflix wameleta uhondo kwenye viganja vyetu unapakua filamu kupitia simu ya mkononi,kompyuta au hata vifaa vingine vyenye uwezo wa kupata mtandao,"

Huku msanii mwenzie Hemed phd ameeleza jinsi ya tamthilia ya Kauli ilivyobeba maudhui ya kitanzania zaidi na kufanya utofauti na tamthilia zingine zinazotumia tamaduni za nje ya nchi.

"Ifike wakati Sanaa yetu wenyewe iwe ndo chanzo kikuu Cha kutangaza utalii,tamaduni na hata lugha yetu kwani mara nyingi tumekua tukitumia vitu ambavyo ni vya wenzetu ila kupitia tamthilia ya Kauli tutaona jinsi ya mipangalio ilivyopangwa kuanzia kwa mtunzi mwenyewe,waandaaji pamoja na waongozaji kwa ujumla.

Hata hivyo hemed amesema zamani wasanii walikua hawawezi kufanya vitu kwa upana zaidi kutokana na kukosa baadhi ya vifaa ili kuboresha kazi zao.

'' Kuongeza kwa Tuzo mbalimbali mfano tuzo za sinema zetu,ziff na nyingine nyingi Ni kipimo tosha kuwa soko la filamu kwa sasa limeimarika na ndio maana wadau wanaleta vitu kama hivo kwa wingi ili kuleta ushindani wa kibiashara kwa wasanii na waandaaji wa filamu".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...