Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) katikati mwenye suti ya kijivu akiwa akiongea na watalamu  wa kitaifa wa Kinga na Udhibiti  wa mionzi kutoka  katika nchi 23 za bara la AFrika waoaohudhuria  mkutano huo unaofanyika jijini Arusha.
 Baadhi ya washiriki wakiwa mkutanoni.
Wataalamu wa kitaifa wa kinga na udhibiti wa mionzi kutoka nchi 23 za bara la AFRIKA akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) mwenye suti ya kijivu mstari wa chini mara baada ya kufungua warsha ya siku tano ya majadiliano ya utekelezaji  wa viwango vya kimataifa  vya kinga na udhibiti wa mionzi vilivyotolewa  mwaka 2014 na Shirika la kimaitaifa la Nguvu za Atomiki Duniani(IAEA).




Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) inaendesha warsha inayohusisha wataalamu wa kitaifa wa kinga na udhibiti wa mionzi kutoka katika nchi 23 kutoka katika Bara la Afrika ambao ni wanachama wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani

Lengo la warsha hii ilionza hivi leo, ni kujadiliana uzoefu wa nchi za Afrika zilizopata kutekeleza viwango vya kinga na udhibiti wa mionzi vilivyotolewa mwaka 2014 na shirika la kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani na pia kujadili changamoto zilizowahi kujitokeza na kuzifanyia marekebisho.

Akifungua mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Prof. Lazaro Busagala amewataka watalaamu hao kujadiliana na kutoa mapendekezo sahihi yatakayosaidia kuwakinga wananchi na mazingira katika nchi zao dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha mionzi katika Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) Bwana Tony Colgan amesema kuwa washiriki wa mkutano huo wanapaswa kujadiliana na kupata mbinu zitakazowezesha kuboresha ulinzi na usalama katika mionzi. Amesistiza kuwa IAEA inapenda kupata mrejesho wa uzoefu wa nchi hizo katika kutumia viwango hivyo vya kimataifa.


Imetolewa na;

Peter G. Ngamilo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...