Shehena
ya Vyavu haramu aina na Makokoro vilivyokamatwa katika Operesheni
inayoendelea katika vijiji vinavyolizunguka bwawa la Nyumba ya Mungu
vikiwa tayari kwa kuteketezwa kwa moto.
Na.Vero Ignatus,Kilimanjaro.
Mkuu
wa Wilaya ya Mwanga Thomas Apson,ameteketeza kwa moto nyavu aina ya
makokoro na vyandarua vya kujikinga na mbu, vinavyotumika kwa uvuvi
haramu vilivyokamatwa katika oparesheni inayoendelea katika vijiji
vinavyolizunguka bwawa la Nyumba ya Mungu vyenye thamani vya
shs.39.3mil.
Apson
amesema kuwa katika oparesheni hiyo wavuvi haramu 14 katika bwawa
hilo wametiwa mbaroni kwa kuwatishia polisi wenye silaha waliokuwa doria
na kuwataka waweke silaha ili wazichape ngumi kavu kavu.
Afisa
Tarafa ya Lembeni Gikila Salisali amesema, baadhi ya watumishi wa
umma wasiokuwa waaminifu wamekuwa kikwazo katika vita hivyo kwa
wanashirikiana na wavuvi haramu na kuiomba serikali iwape boti ili
kuimarisha doria ndani ya bwawa.
Wananchi
wa vijiji hivyo bi Eda Eliakimu na bakari kingazi wakazi wa nyumba ya
Mungu wameipongeza serikali kwa kutangaza upya vita hivyo ambavyo
wamesema vinaweza kusaidia kupunguza kasi ya uvuvi haramu ambao umekuwa
tishio kwa samaki wachanga ambao wangeweza kubadili maisha yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...