Na Mwandishi wetu Glou ya Jamii
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam leo, ambao ni Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali, Katibu Tawala, Balozi, Kamishna wa kazi katika ofisi ya Waziri Mkuu, na Majaji 12 wa mahakama kuu pamoja na Mwenyekiti, na makamu mwenyekiti na Makamishna watano wa Tume ya Haki za binadamu na utawala bora.

Akizungumza na viongozi hao wateule, Rais Magufuli amesema kuwa walioteuliwa wasidhani kuwa hizo ndio nafasi zao moja kwa moja, Pia amewashauri majaji wakafanye kazi kwa haki bila kumuonea Mtu, kwani hukumu hutolewa na Mungu tu, ila kwa hapa duniani tunao Majaji.
"Kuna watu ukiwateua wanadhani hizo ndio nafasi zao moja kwa moja, wewe (CAG) nilipokutoa toka kuwa Mkurugenzi wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) kwenda kuwa Katibu Tawala mkoa hukusema neno na ulikuwa mtulivu ,wapo wengine ukiwatoa wanasema maneno maneno, wakati huo unapowateua huwa hawasemi" Amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amemuasa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutokuwaonea watu pale anapopewa maagizo na mihimili mingine kama Bunge na Mahakama, akatekeleze majukumu yake kwani yeye ni mtumishi na asibishane.
"Najua CAG una 'Qualification' nzuri tu na huwa hatufanyi makosa tunapoteua, form four ulitoka na divison one, form six ukatoka na division one hii ni kuonesha wewe ni kipanga sio kilaza, 'Degree' ya sheria unayo, ukachukua na masters, umefanya kazi sehemu nyingi tu" Amesema Rais Magufuli.
Rais Dkt John Pombe Magufuli leo Novemba 4,2019 amemuapisha Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufuatia uteuzi alioufanya hapo jana. Hafla ya kumuapisha Kichere ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe pamoja na viongozi wengine, imefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...