Taasisi ya CCBRT Tanzania imetimiza miaka 25 ya kutoa huduma za tiba kwa watoto wenye matatizo ya macho, miguu pinde, mgongo wazi na afya ya uzazi ikiwemo fistula.
Akizungumza
na waandishi wa habari na wageni waalikwa, Rais wa bodi ya CCBRT
Tanzania, Dkt. Wilbrod Slaa alisema tulianzisha hospitali ya CCBRT mwaka
1994 mwezi wa Nne tukiwa na malengo ya kusaidia watoto wenye ulemavu,
lakini wazo lilikuja nikiwa na Dan Wood tukiwa Zanzibar baada ya ajali
ya ndege iliyotokea Rwanda
"
Nakumbuka mwanzo tulikuwa tunapita mitaani kwenye nyumba na kukuta
watoto wenye matatizo ya miguu na macho, kuna nyumba tulikuta mtoto
ambaye alikuwa hana uwezo wa kuona mchana lakini usiku anaona vizuri
wataalamu wanakumbuka , huyu ndio alikuwa mgonjwa wetu wa kwanza".
alisema Slaa. Kina mama wengi ilikuwa tukipita mitaani walikuwa wanalia
kuomba msaada wa watoto wao wenye matatizo mbalimbali na tuliweza
kuwasiadia
Tulipata
changamoto ya kupata sehemu ya kufanyia operesheni, ikabidi tuende
hospitali ya Mwananyamala na kuomba kupewa ruhusa ya kuwafanyia
operesheni wagonjwa wetu wakaturuhusu na changamoto nyingine ilikuwa
mahali pa kulaza wagonjwa wetu, na ilibidi tukiuke taratibu na kwenda
kuwapangishia kwenye nyumba ya kulala wageni ambazo tulikodi kwa
wagonjwa tu, na kwa bahati waziri wa afya kipindi hicho, mhe. Anna
Abdallah alitoa baraka zake wagonjwa waweze kuwekwa kwenye nyumba hiyo.
Aliendelea kusema Dkt. Slaa
Tunashukuru
serikali ya Tanzania kuwa mdau mkubwa sana wa CCBRT kwa kutoa ardhi
kubwa bure kuwezesha kujenga hospitali na kupandisha hadhi hospitali
yetu kuwa ya rufaa (zonal referral) alisema Dkt. Slaa
Pia
tunatoa huduma zetu kulingana na wagonjwa tunaowapokea, hii inategemea
mgongwa private au sio private na gharama tunazowachaji wagonjwa wa
private zinaenda kutibia wagongwa wasio na uwezo gharama za matibabu
alimaliza kusema Dkt. Slaa
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, alisema, Naomba kuchukua nafasi hii kuwapongeza Taasisi ya CCBRT kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake nchini. Najua mmepitia changamoto nyingi sana pindi mlipoanza kama alivyokwisha kusema Rais wa bodi ya Taasisi ya CCBRT Dkt. Wilbrod Slaa.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, alisema, Naomba kuchukua nafasi hii kuwapongeza Taasisi ya CCBRT kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake nchini. Najua mmepitia changamoto nyingi sana pindi mlipoanza kama alivyokwisha kusema Rais wa bodi ya Taasisi ya CCBRT Dkt. Wilbrod Slaa.
Pia
niwapongeze kwa kuwa na huduma za mkoba (mobile outreach) ambazo
zimekuwa na ubia na hospitali mbalimbali nchini kama vile Bombo mkoani
Tanga, Seko Toure Mwanza, Mnazi Mmoja Zanzibar, Kabanga Kigoma, Bagamoyo
na Ikwiriri hii inaonyesha jinsi gani mmeweza kuwa bega kwa bega nasi
serikali alisema Mhe. Mwalimu.
Nachukua
fursa hii pia kuwapongeza, kituo cha CCBRT Moshi ambacho kinafanya kazi
nzuri sana, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996 kimeweza kuhudumia watoto
wenye ulemavu na familia zao zaidi ya 10,000 na kuwarejeshea matumaini
aliendelea Mhe. Mwalimu
Nimepewa
taarifa CCBRT ndani ya miaka 9 mnashirikiana na timu ya usimamizi na
uendeshaji wa huduma za afya mkoa wa Dar es salaam kutoa mafunzo kwa
watoa huduma zaidi ya 900 kila mwaka hasa kwa madaktari na wauguzi. Na
mradi wa kuwajengea uwezo watumishi kwenye vituo vya afya na zahanati 22
katika manispaa zote tano za mkoa wa Dar es salaam na Pia mradi huu
umewekeza kiasi kikubwa cha miundombinu, ukarabati wa wodi za wazazi,
ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 1,895,615,400
na uwekezaji wa vyumba maalum vya watoto njiti, vyoo maalum kwa wenye
ulemavu, utambuzi wa mapema wa watoto wenye ulemavu na kina mama wenye
fistula ya uzazi aliendelea kusema Mwalimu.
Kwenye
fistula wastani ya akina mama 800 kwa mwaka walipata huduma ya
upasuaji, takwimu zinaonyesha akima mama takribani 2000 hadi 3000 hupata
fistula ya uzazi nchini , CCBRT kushirikiana na MUHAS, Chuo kikuu
Dodoma, KCMC kumewezesha kutoa mafunzo na Taasisi ya kimataifa ya
madaktari bingwa magonjwa ya kinamama na wajawazito,(figo) kuwa miongoni
mwa vituo vya mafunzo ya upasuaji fistula duniani, na mpaka kufikia
mwezi 10 mwaka 2019 watakuwa wamefanya upasuaji fistula kina mama
wapatao 10,000 alimaliza kusema.
Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kwa kununua picha iliyouzwa kwenye mnada kwa thamani ya shilingi millioni 4.5 huku Dkt. Wilbrod Slaa akimpongeza mmoja kati ya wafanyakazi wa benki hiyo.Taasisi ya CCBRT Tanzania imetimiza miaka 25 ya kutoa huduma za tiba kwa watoto wenye matatizo ya macho, miguu pinde, mgongo wazi na afya ya uzazi ikiwemo fistula.
Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kwa kununua picha iliyouzwa kwenye mnada kwa thamani ya shilingi millioni 4.5 huku Dkt. Wilbrod Slaa akimpongeza mmoja kati ya wafanyakazi wa benki hiyo.Taasisi ya CCBRT Tanzania imetimiza miaka 25 ya kutoa huduma za tiba kwa watoto wenye matatizo ya macho, miguu pinde, mgongo wazi na afya ya uzazi ikiwemo fistula.
Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akizungumza na wageni waalikwa kwenye tafrija ya maadhimisho ya miaka 25 ya
taasisi ya hospitali ya CCBRT jana
jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda Msangi
akizungumza na wageni waalikwa
Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa
kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa PWC kwa kununua picha iliyouzwa kwenye
mnada kwa thamani ya shilingi millioni 2 ili kuchangia gharama za matibabu kwa
wasiojiweza
Rais wa bodi ya Taasisi ya hospitali ya CCBRT, Wilbrod Slaa akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda
Msangi
Rais wa bodi ya Taasisi ya hospitali ya CCBRT, Wilbrod Slaa (kulia) akimkabidhi picha
ya zawadi kwa mchango alioutoa kwa taasisi hiyo Makamu wa zamani wa Rais bodi
ya CCBRT, Biharilal Tanna , kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt.
Brenda Msangi
Baadhi ya wakina mama waliopokea vyeti vya kutambua mchango
wao kwa CCBRT wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa
CCBRT, Dkt. Brenda Msangina Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Dkt. Brenda
Msangi
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye tafrija ya CCBRT usiku wa
jana
Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wapili
kushoto waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa bodi ya Taasisi ya hospitali
ya CCBRT, Wilbrod Slaa (wapili kulia waliokaa) Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa
CCBRT, Dkt. Brenda Msangi na Makamu wa Rais wa zamani wa bodi hiyo, Biharilal
Tanna na wadau mbalimbali kwenye tafrija ya maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi
ya hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa
kwenye picha ya pamoja na viongozi na
wafanyakazi wa Taasisi ya hospitali ya CCBRT jana kwenye tafrija ya
maadhimisho ya miaka 25 ya taasisi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...