Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk Thomas Rutachuuzibwa wa tatu kutoka kushoto mstari wa kwanza akiwa na kamati ya Usimamizi wa Afya ya Mkoa wa MWanza na Mkuu wa ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania,Bwana Miguta Ngulimi wakiwa katika picha ya pamoja mara baaada ya kupata matokeo ya ukaguzi uliofanyika katika mkoa wa Mwanza.


Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) katika ukaguzi wake wa kawaida wa kila mwaka umevifungia vituo vitatu vya afya kutoa huduma ya mionzi (X-ray) kutokana na kutokidhi matakwa ya Sheria Na. 7 ya Nguvu za Atomiki ya Mwaka 2003 na kwamba vitarejeshewa huduma hiyo mara vituo hivi vitakaporekebisha mapungufu yaliyoonekana. 

Vituo vilivyofungiwa ni vya Wilaya ya Sumve, Hospitali ya Wilaya ya Ngudu na Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.

Vituo hivyo vimefungwa kufuatia ukaguzi unaoendelea mkoani Mwanza ikiwa ni zoezi linalofanyika kila mwaka katika kuhakikisha usalama wa utoaji wa huduma ya mionzi unafuatwa kama ambavyo ilivyoelekezwa katika Sheria Na. 7 ya Nguvu za Atomiki Tanzania ya Mwaka 2003 ili kulinda wafanyakazi, wagonjwa, wananchi na mazingira dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi. Katika vituo vya Sumve na Ngudu imegundulika kuwa watumishi wake hawana sifa za upigaji wa picha za mionzi huku katika kituo cha Misungwi imegundulika kuwa vifaa vyao vya mionzi havina ubora unaostahili.

TAEC inavitaka vituo vyote vinavyotumia mionzi katika utoaji wao wa huduma mbalimbali kuhakikisha vinafuata Sheria na taratibu za kiusalama kama ilivyoelekzwa katika sheria ikiwemo kuishirikisha TAEC katika hatua zote za ujenzi wa vituo hivyo kwa lengo la kulinda afya za Watanzania.

Katika ukaguzi huu unaoendelea jumla ya Vituo 32 vimekaguliwa ambapo vituo 28 ni vya sekta ya afya na vituo 4 ni katika sekta ya viwanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...