Na Mwandishi wetu,Mtwara
WAKATI wakulima wa korosho wakiendelea na
msimu mpya wa korosho kwa mwaka 2019/20 Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)
imesema itaendelea kuwahudumia na kuwahakikishia usalama wa fedha zao huku
ikisogeza huduma hizo karibu zaidi badala ya kusafiri umbali mrefu.
Akizungumza wakati wa Kongamano la Uwekezaji
na Maonyesho ya Biashara mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki, Meneja wa NBC Mkoa wa
Mtwara, Job Nshatsi alisema wameendelea kuwa mstari wa mbele kutuoa huduma za
kibenki, ushauri na mafunzo ya kifedha na biashara yanayowezeha wateja wake
ikiwemo wakulima na wafanyabiashara wa korosho.
Alisema katika kuhakikisha wakulima
wananufaika na huduma zake tayari wameendelea kuongeza mtandao wao wa mawakala
katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wakulima wanapata fedha kwa wakati
lakini pia kwa usalama kwa kuepuka kusafiri na fedha umbali mrefu kwenda palipo
na tawi la benki hiyo.
“NBC tunatoa huduma za kibenki maalumu kwa
ajili ya kukuza na kuendeleza kilimo-biashara (agribusiness) kwa kushirikiana
na Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kilimo nchioni (PASS), tukiangalia sekta ya
kilimo na mnyororo mzima wa thamani katika kilimo, na kwa Mtwara tutaendelea
kutoa huduma ili kusaidia kukuza uzalishaji, uongezaji wa thamani na uuzaji wa
zao la korosho,”alisema Nshatsi
Aidha alisema NBC kwa kushirikiana na Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wanaendelea kutoa elimu za
kifedha kwenye vikundi mbalimbali vya wajasiriamali lengo ikiwa ni kuwawezesha
wajasiriamali hao kupata mbinu mbalimbali katika kuendesha biashara zao.
Nshatsi alizidi kueleza kuwa ili kuhakikisha
watu wengi wanafikiwa na huduma za kibenki wamerahisisha ufunguaji wa akaunti
kupitia akaunti ya NBC Fasta ambapo mteja anahitajika kuwa na kitambulisho
kimoja au barua ya mtendaji na kufunguliwa akaunti.
Wakizungumza baadhi ya wananchi waliohudhuria
kongamano hilo waliziomba taasisi za kifedha kuendelea kuwapa elimu ya matumizi
sahihi ya fedha hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mavuno ya korosho.
“Tunapohudhuria makongamano tunatumaini
tutapata elimu mbalimbali lakini watu wa benki waendelee kutoa elimu ya
matumizi sahihi ya fedha ili kuwa
endelevu hasa kipindi hiki ambacho wakulima wanauza korosho wasaidiwe wajue
baada ya kuuza fedha wanazozipata wanatakiwa kuziendeleza kwenye miradi mingine
ya maendeleo,”alisema Asha Chimae
Naye mwanachi mwengine Hansi Chilumba alisema
“Wananchi wapo tayari kufanya kazi lakini kinachokosekana ni ujuzi na mtaji, ni
vizuri benki kuendelea kutuwezesha hata mmoja mmoja ili kutimiza malengo kwa
sababu kila mtu anakuwa na malengo yake lakini tunapounda kikundi inakuwa ngumu
kwa wote kukubali wazo la mmoja ili kulifanyia kazi.
Ofisa Huduma Wateja wa Benki ya NBC Tawi la Mtwara, Lulu
Mutayoba (katikati), akitoa maelezo kuhusu huduma za kibenki zotolewazo na NBC
wakati wa Kongamano la Uwekezaji na Maonyesho ya Biashara Mtwara yakiyofanyika
katika Viwanja vya Chuo cha Elimu Mtwara mwishoni mwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...