Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto), akifurahi mara baada ya kufunua pazia kuzindua mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kwenye Hoteli ya Coral Beach, Dar es Salaam Mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo na Rais wa Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka na kutoka kulia ni Woinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42. Mashindano hayo yatafanyika Machi Mosi mwakani. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto), akifunua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kwenye Hoteli ya Coral Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo na Rais wa Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka na kutoka kulia niWoinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto), akikabidhiwa zawadi na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42.
Meneja wa Grand Malt, David Tarimo wadhamini wa mbio za Km 5, akielezea kuhusu udhamini huo pamoja na sifa za kinywaji hicho.
Woinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon akielezea kuhusu udhamini wao na kuwaomba watanzania kuisapoti kampuni hiyo kwa kujisajili kwa wingi kujiunga na mtandao huo mkubwa nchini. 
Pamela Kikuli Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42. zielezea kuhusu udhamini wa mbio ndefu na kuitangaza bia ya Kilimanjaro yenye jina linalotukuza Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio kikubwa cha utalii nchini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Executive Solutions Waratibu wa mashindano hayo akiongoza hafla hiyo ya uzinduzi na kuelezea umuhimu wa watu kuanza kujisajili ili kushiriki mashindano hayo makubwa nchini na nje ya Nchi.
RAIS WA TOC, FILBERT bAYI AKIELEZEA UMUHIMU WA WATANZANIA KUSHIRIKI NA KUSHINDA MASHINDANO HAYO, ILI WAPATE FURSA YA KUSHIRIKI MASHINDANO YA OLIMPIKI.
Rais wa RT, Anthony Mtaka akitangaza nyongeza ya bonasi kwa wanariadha watanzania watakaoshinda mashindano hayo.
Waziri Dk. Mwakyembe akihutubia katika hafla hiyo
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leodger Tenga akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
Waziri Dk. Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa RT, BMT na wadhamini wa mashindano hayo
Waziri Dk. Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa RT, BMT na wadhamini wa pamoja na waandaji na waratibu wa Kilimanjaro Marathoni.




Na Richard Mwaikenda 

WANARIADHA wa Tanzania watakaoshinda mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kuibuka na kitita cha sh. mil. 7 ambapo sh. Mil 4 ni zawadi ya kawaida na sh. mil 3 ni motisha.

Motisha hiyo ilitangazwa na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano hayo, uliofanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika Hotel ya Coral Beach, Masaki, Dar es Salaam jana.

Waziri Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema kuwa motisha hiyo iwe ni kichocheo kikubwa kwa wanariadha wa Tanzania kushiriki kwa wingi na kushinda mbio hizo.Alisema kuwa huwa inashangaza kuona zawadi ya 1-39 zinakwenda kwa wakimbiaji wa kutoka nje, wakati Tanzania ina watu wenye misuli, mikono na vifua lakini hushindwa, wakati watu hao hao wakikimbizwa na polisi hukimbia sana.

“Nitafurahi sana kuona bahasha nyingi za zawadi zikibaki nchini, naomba wenye uwezo mkubwa tushiriki kwenye mbio hizi zenye jina kubwa kimataifa,” alisema Dk.Mwakyembe.Aliwapongeza waandaji wa mashindano hayo ambayo sasa yamekuwa yanavutia watu wengi kutoka mataifa 56 Ulimwenguni, hali inayochangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania.Alisema kitendo hicho kimesaidia sana kuutangaza Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine vya utalii vilivyopo nchini. Pia imesaidia mashindano hayo kuwa na wadhamini wengi.

Rais wa RT, Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, aliwaasa wanariadha wa Tanzania kuachana na kasumba ya kukimbilia kushiriki mashindano ya nje ambako hata zawadi wanazopewa ni sawa na zinazotolewa na Kilimanjaro marathoni na mara nyingine kuzidi.

Aliwataka wajenge tabia ya kupenda kushiriki mashindano ya nyumbani na hasa Kilimanjaro Marathon yenye hadhi kubwa sawa na mengine ya kimataifa. Alisema kuwa waandaji wameamua kutoa motisha ili wanariadha wa kitanzania washiriki kwa wingi na kushinda.

Alisema kuwa wanariadha wakienda nje kushiriki baadhi hulipwa dola 1000 ambayo ni sawa na sh. 2,460,000 za Tanzania na wengine hulipwa dola 500, kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na zawadi ya sh. mil. 4 na nyongeza ya motisha sh. mil. 3, jumla sh. mil 7 kwa mshindi wa mbio za Km 42.

Mshindi wa Tigo Kili Half Marathon Km 21, hulipwa sh. mil. 2 kwa upande wa wanaume na wanawake pia.Mashindano hayo mwaka huu yametimiza miaka 18 tangu ilipoanzishwa 2001.Naye, Rais wa Kamati ya Olympic Tanzania TOC, Filbert Bayi, alisema kuwa wanariadha inabidi wayathamini mashindano ya Kilimanjaro Marathon, kwani ni kipimo tosha cha washindi kupata fursa ya kushiriki mashindano ya Olympic Tokyo, Japan 2020.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leodger Tenga, alisema hakuna njia ya mkato katika mafanikio, hivyo kuwataka wanariadha kutobweteka, bali wajitahidi sana kufanya mazoezi ambayo ni msingi wa mafanikio ya ushindi.

Hafla hiyo iliwakilishwa pia na Pamela Kikuli Meneja wa Bia ya Kilimanjaro wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42, Woinde Chisael Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo inayodhamini mbio za Km. 21 na David Tarimo Meneja wa kinywaji aina ya Grand Malt wadhamini wa mbio za Km. 5.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...