Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UONGOZI wa Yanga umevunja mkataba na kocha wake Mwinyi Zahera, benchi la ufundi  na kuvunja kamati ya mashindano.

Kwa habari za Uhakika, Zahera anadai takribani Dola 60,000 sawa na Milion 130 za Kitanzania zikiwa ni za Malipo ya mkataba unaoisha Septemba 2020,  akidai mshahara na marupurupu mengine.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt Mshindo Msolla akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Klabu.

Akielezea maamuzi hayo, Msolla amesema wamefikia maamuzi hayo baada ya kufikia makubaliano na Kocha Mkuu na benchi la ufundi la kuamua kuvunja mkataba.

Amesema, kwa sasa timu itakuwa chini ya Kaimu Kocha Charles Boniface Mkwasa mpaka pale kocha Mkuu atakapotangazwa tena

Aidha, Zahera hakuwa anafahamu kama kibarua chake kimeota nyasi na mpaka kufikia asubuhi ya leo amefika mazoezini kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini na kuendelea na majukumu yake wakati timu yake ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda ya Mtwara.

Yanga inasafiri kesho kuelekea Mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ndanda utakaopigwa siku ya Ijumaa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Timu hiyo itasafiri na benchi jipya la  ufundi likiongozwa na Mkwasa, akisaidiwa na Said Maulid na wengineo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...