Na, Editha Edward-Tabora .
Halmashauri  ya Manispaa ya Tabora inatarajia Kutumia zaidi ya Shilingi bilioni mbili kufanya ukarabati mkubwa wa machinjio ya mifugo mjini Tabora baada ya kukamilisha nyaraka za upembuzi yakinifu kwa mwaka wa fedha 2019/2020 
Wajumbe wa kamati ya fedha halmashauri ya manispaa ya Tabora wametembelea machinjio hayo ya mkoa wa Tabora na kuweza kujionea kile ambacho tayari walisomewa na wataalam kwenye nyaraka za upembuzi yakinifu ya kuomba fedha hivyo wa ajili ya ukarabati mkubwa wa machinjio hayo
Nae Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Joseph Kashushula amewaeleza Wajumbe wa kamati hiyo ya fedha hatua za mwanzo zilizotumika  za kufanya ukarabati mdogo wa machinjio  hiyo kuwa uligharimu zaidi ya shilingi milioni kumi na tano  huku akisema mapato  yatokanayo na tozo ya machinjio hiyo ambayo kwa  siku inachinja kati ya ng'ombe  sitini na tano hadi Sabini
"Tuna mipango mizuri ya kuhakikisha kwamba machinjio hii tunaikarabati na inakuwa ni ya kusasa zaidi tunategemea kupata pesa kutoka central government au kama itakuwa Siyo huko tutaweza kupata fedha kwa wafadhili na tayari maandiko tumeshaandika"Amesema Kashushula
Kwa upande wake Naibu meya wa manispaa ya Tabora Hahaha Muhamali amesisitiza umuhimu wa chanzo hicho cha mapato ya ndani ya halmashauri "sasa hivi tunatengeneza  hizi kuta tunazowekea tailizi lakini hizi sakafu Siyo salama kiafya kwa Sababu nyama zinakaa chini haziko katika hali nzuri mimi nadhani tutajadili kwenye kikao chetu tutajadili tuone ni jinsi gani tuweze kufanyia ukarabati na hii sakafu"Amesema Muhamali 
Aidha machinjio hiyo ya  manispaa ya Tabora imekuwa ikiingiza mapato ya wastani wa Shilingi milioni kumi na laki tano kwa mwezi kwa tozo ya uchinjaji wa ng'ombe pekee ukiachilia mbali na makusanyo ya tozo ya ushuru wa damu baada ya ng'ombe kuchinjwa.

Muonekano wa machinjio kwa ndani ambayo hapo awali yalikarabatiwa kwa kiasi cha shilingi milioni kumi na tano. 
Wajumbe wa kamati ha fedha halmashauri ya manispaa ya Tabora wakitembelea machinjio hayo ya mkoa wa Tabora. 
Wajumbe wa kamati ya fedha halmashauri ya manispaa ya Tabora wakiwa ndani ya machinjio hayo wakielekezwa jambo





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...