Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
leo imetangaza na kuzindua kampeni maalum ambayo inayojulikana kama LIPA ADA kwa Airtel Money
itakayotoa suluhisho kwa wateja wake kuweza kufanya malipo yoyote
ya karo za shule ambapo kwa sasa wateja wataweza kulipa karo kwa kutumia
akaunti zao za Airtel Money wakiwa popote katika kipindi hiki cha
msimu wa sikukuu na kuendelea.
Akizungumza leo
jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza kampeni hiyo, Mkurugenzi wa
Airtel Money Isack Nchunda alisema kuwa LIPA ADA kwa kutumia Airtel
Money itakuwa ni suluhisho
kwa wazazi wengi ambao wamekuwa wakipoteza muda mwingi wa kwenda
kupanga foleni benki ili kulipia watoto wao karo na vile vile itaendela
kutoa hamasa kwa wateja wa Airtel kuendelea kutumia Airtel Money kulipia
malipo mbali mbali ya bidhaa na huduma.
‘Kama mnavyojua,
hiki ni kipindi cha wazazi na familia kuwa katika mapumziko, lakini pia
muda huu wazazi huutumia kulipia karo za shule za watoto wao. Natoa wito
kwa Watanzania
kuendelea kutumia Airtel Money kwa malipo yao kwani ni njia rahisi,
haraka na nafuu kwa malipo wakiwa popote wanaweza kulipa sio lazima
kwenda bank na kupanga foleni, Nchunda alisema.
Nchunda alisema kuwa
Airtel imeamua kuja na kampeni ya LIPA ADA kwa Airtel Money kama njia
mojawapo ya kutoa suluhisho ya kifedha kwa Watanzania. ‘Kama mnavyojua,
kulingana na
utafiti wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wa hivi karibuni
kuonyesha kuwa zaidi ya Watanzania milioni 22.9 wanatumia huduma za
kifedha kwa kutumia simu zao huku miamala yenye dhamani ya zaidi ya
Trilioni 8 ikifanyika mpaka kufikia Juni 2019. Kwa miaka
ya hivi karibuni, huduma za kifedha kwa simu za mkononi imebadilika
kutoka huduma ya kawaida kama vile kununua muda wa maongezi mpaka kuwa
moja ya huduma muhimu inayowezesha ukuaji sekta na mzunguko wa fedha
kila mahali.
Jinsi ya kulipia Ada Kwa Airtel Money:
- Piga *150*60# Ili kufikia Kwenye Menyu ya Airtel Money
- Chagua 5: Lipia Bili
- Chagua 4: Weka namba ya kampuni (Namba ya Malipo ya Shule)
- Ingiza Kiasi cha pesa
- Ingiza Namba ya Kumbukumbu (Jina la mwanafunzi na Kidato / Namba ya kitambulisho cha mwanafunzi )
- Ingiza Namba ya siri
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema
kuwa Airtel inajivunia kuwa kampuni ya simu za mkononi ambayo sasa inakuza kwa kasi mtandao wa huduma za kifedha hapa nchini.
“Airtel tumejipanga
na kujikita katika mipango yetu ya kuendelea kupanua wingo wa huduma
zetu, Airtel kwa sasa tuna maduka ya Airtel Money branches Zaidi ya 1000
nchi nzima ikiwa
ni moaja kati ya mpango yetu ya kuleta suluhisho za kifedha pamoja na
kusambaza huduma na bidhaa zetu karibu na wateja. Dhamira yetu ni
kuendelea kujenga mtandao imara na unaotegemewa’. Alisema Singano huku
akiongeza kuwa huduma na bidhaa za Airtel kama vile
kurundisha muamala uliokosewa, kubadilisha PIN, kusajili laini za simu
kwa kutumia alama ya vidole zinapatikana kwenye maduka yote ya Airtel
Money branches.
Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda akizungumza wakati wa kuzindua kampeni maalum inayojulikana kama LIPA ADA kwa Airtel Money
itakayotoa suluhisho kwa wateja wa Airtel Money kuweza kufanya malipo
yoyote ya karo za shule kwa kutumia akaunti zao za Aitel Money wakiwa
popote katika kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu na kuendelea Kushoto ni Meneja wa Airtel Jackson Mmbando
Meneja wa Airtel Jackson Mmbando akifafanua jambo wakati wa kuzindua kampeni maalum inayojulikana kama LIPA ADA kwa Airtel Money itakayowawezesha
kwa wateja Airtel kuweza kufanya malipo yoyote ya karo za shule kupitia
akaunti zao za Aitel Money wakiwa popote wakati msimu huu wa Sikukuu na
kuendelea, hafla ya uzinduzi ilifanyika ofisi kuu ya Airtel jijini Dar
es Salaam jana.Katikati ni Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda na
kulia ni Mkuu wa Kitengo cha lipa Ada kwa Airtel Money. Emmanuel
Mwaisoloka
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...