Uzio wa Bandari ya Nyamirembe ukiwa umeshakamilika kama sehemu ya kuimarisha usalama bandarini hapo baada ya ujenzi wa miundombinu yake kukamilika.
 Baadhi ya nyumba za zamani ambazo zilikuwa zinatumiwa na watumishi wa Bandari ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita.
 aadhi ya mafundi wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa kuhusu ujenzi wa bandari ya Nyamirembe kutoka kwa Meneja wa TPA Bandari za Ziwa Victoria Morric Mchindiuza (PICHA ZOTE NA SAIDI MWISHEHE-CHATO)
 Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa gati lililojengwa katika bandari ya Nyamirembe wilayani Chato ikiwa ni mkakati wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari(TPA) kuboresha miundombinu ya ya bandari za Viwa Victoria
 Muonekano wa gati ya Bandari ya Nyamirembe wilayani Chato ambapo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100 awamu ya kwanza na mkakati wa Mamlaka ya Bandari ni kuanza ujenzi wa awamu ya pili ya gati hiyo ili kuosogeza kwenye kina kirefu cha maji kwa ajili ya meli kubwa kuweza kushusha na kupakia abiria pampoja na mizigo.
 Mafundi wakiendelea na ujenzi wa gati ya Bandari ya Nyamirembe ambayo tayari imekamilika kwa awamu ya kwanza.
 Sehemu ya muonekano wa gati ya Bandari ya Nyamirembe baada ya kukamilika kwa ujenzi wake.
 Mhandisi Anderson Robert Ndogae akizungumza waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa gati ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita.
 Moja ya jengo la Bandari ya Nyamirembe likiwa limekamilika ikiwa ni mkakati wa ujenzi wa miundombinu katika bandari hiyo kwa ajili ya kuboresha usafiri wa meli Ziwa Victoria.

Said Mwishehe Michuzi Globu ya jamii -Chato

IMEELEZWA kwamba hatua ya Mamlaka ya Usimami Iwa Bandari Tanzania (TPA), kukamilisha ujenzi wa Bandari ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita, sasa kutafungua milango ya usafirishaji wa mzigo na shughuli za utalii nchini. 

Pia imeelezwa bandari hiyo itakapokamilika itakuwa ni uwezo wa kusafirisha mizigo katika nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuanzia Machi mwaka 2020 baada ya kukamilika kwa meli zinazoendelea kujengwa na nyingine kufanyiwa matengeneza makubwa katika Ziwa Victoria. 

Hayo yameelezwa na Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Morris Machindiuza alipokuwa akielezea hatua za ujenzi wa bandari hiyo ambapo tayari baadhi ya majengo yamekamilika huku awamu ya kwanza ya gati nayo ikiwa imeshamilika licha ya kuwepo kwa awamu ya pili ya ujenzi wa gati hiyo ili kuosegeza kwenye kina kirefu cha maji kwa ajili ya meli kubwa kuweza kushusha na kupakia mizigio na abiria.

Amefafanua kuwa Bandari ya Nyamirembe ni mlago muhimu kwa uchumi wa Ziwa Victoria kwani kwa muda mrefu ilikuwa na manufaa kwa wananchi na wasafirishaji wa mizigo na kuchochea maendeleo huku akisisitiza kuwa bandari hiyo ni muhimu kwa TPA na wananchhi kwa ujumla hasa.

"Historia ya Bandari ya Nyamirembe ni kwamba ilianza kufanyakazi mwaka 1960 na tangu wakati huo ilikuwa chini ya Shirika la Reli Tanzania(TRC).Hata hivyo kutokana na mabadiliko ilipofika mwaka 1997 ilikabidhiwa kwa Kampuni ya Huduma za  Meli na tangu wakati huo zipo meli zilikuwa zikifika hapa na kutia nanga na ambayo ilikuwa na uwezo wa kuibeba abiria 593 na kuibeba tani 350,"amesema.

Ameongeza kuwa na meli hiyo ilikuwa ikibeba mazao mbalimbali yakiwamo ya pamba, mchele na kwamba  ilikuwa kama daladala katika maeneo yote muhimu ilikuwa inasimama kuchukua abiria na mizigo. "Na sasa TPA kutokana na umuhimu wake tuliwekeza na kuiuhisha kwa kuanza ukarabati wake kwa gharama za za Shilingi bilioni 4.128 kwa kuhusisha ujenzi wa gati,mnara wa meli na  jengo la abiria.

Mchiundaza amesema kuwa bandari hiyo sasa itakwenda kuchochea utalii na hiyo inatoka na uwepo wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato, Rubondo ambapo pia shughuli za utalii zitaongezeka.

 "Tuna matarajio makubwa ya kuongezeka kwa watalii ambao watakuja kwenye hifadhi yetu mpya ya Burigi -Chato, hivyo kwetu sisi TPA ni fursa nyingine ya kibiashara kwani wengi watapenda kutumia usafiri wa meli kuja huku na kwa kukumbusha tu kusafiri kwa meli nako ni sehemu ya utalii na wengi watapenda."
Mwisho
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...