Na
Said Mwishehe, Michuzi TV-Kigoma
MAMLAKA
ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) umesema unatekeleza miradi 27 yenye
thamani ya Sh.bilioni 123.345 katika Bandari za Ziwa Tanganyika ukiwa ni
uwekezaji mkubwa kupata kutokea nchini katika ukanda huo wa ziwa hilo.
Hayo
yameelezwa na Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Percival Salama wakati
akizungumza na waandishi wa habari walioko kwenye ziara ya kukagua miradi
mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu katika bandari za maziwa makuu
unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya
Bandari(TPA).
Akizungumza
zaidi kuhusu miradi hiyo na hasa kwa kuanza na Mkoa wa Kigoma Salama amesema kiwango hicho cha fedha
ambacho kimewekwa katika kutekeleza miradi hiyo katika Bandari za Ziwa
Tanganyika kinaonesha dhahiri dhamira njema ya Serikali ya Awamu ya Tano
kusogeza huduma za bandari karibu na wananchi na kubwa zaidi TPA inatambua
umuhimu wa miundombinu ya bandari iliyoboreshwa katika maeneo yote yenye maziwa
makuu.
Amesema
kwa upande wa Mkoa wa Kigoma wameendelea kutekeleza miradi ya kimkakati ambapo
amefafanua kuna mradi mkubwa unaondelea ukiwemo wa kujenga miuombinu ya bandari
ya Kibirizi, Bandari ya Ujiji pamoja na ofisi mpya ya Meneja wa Bandari.
"Mradi
huu unatekelezwa na mkandarasi CR15G China Ralway Cooperation na ndio tumeingia
naye mkataba wa miezi 24 na ameanza kazi Machi 5, mwaka 2019, mradi huu una
gharama ya Shilingi bilioni 32. 525.Ni uwekezaji mkubwa ambao unakwenda
kubadili mazingira na muonekano mpya wa bandari kwenye Mkoa wa Kigom, kwa hiyo Bandari ya Kibirizi tunajenga gati
ya urefu wa mita 250.
"Pia
tunajenga mashed matatu makubwa, eneo la kupumzikia abiria, ofisi na
miundombinu mengine wezeshi ambayo itafanya bandari hii ya majahazi kuwa nzuri
na inayoweza kutoa huduma zinazotakiwa. Lakini tuna jengo la Meneja wa Bandari amba;o
ujenzi wake tayari umeanza , ni jengo zuri bora na ramani yake ni nzuri ambayo
nayo ipo ndani ya mradi wa Kibirizi,"amesema.
Ameongeza
kuwa Bandari ya Ujiji wanatengeneza gati ya urefu wa mita 110 na kwamba Ujiji
ni mji wa kihistoria ambako katika bandari hiyo wanajenga miundombinu ikiwemo
eneo la chakula, sehemu ya kupumzikia abiria, maghala ya mizigo na kwamba huo
ni mradi mmmoja ambao unatekelezwa ndani ya Mkoa wa Kigoma.
"Mradi
wa pili ambao unatekelezwa na wakandarasi wawili kwa wakati mmoja Satellite
pamoja na Josam ni mradi wa ujenzi wa Bandari Kavu ya Katosho ni mradi mkubwa
wa Sh bilioni 2.9 unatekelezwa kwa muda wa miezi tisa na sasa hivi wako karibu
asilimia 80 ya utekelezaji.Kimsingi tunatarajia ifikapo Desemba 27, mwaka 2019
wakatabidhi mradi na kwa kasi ambayo wanakwenda nayo tunaamini kabisa kufika tarehe
hiyo wataukabidhi kwani ulianza
kutekelezwa Machi 28,2019, kwa hiyo utaona tulianza kwa kusuasua lakini
kuanzia Agosti ulikuwa asilimia 10 ya utekelezaji ambapo hadi sasa wamefanya
kazi kwa asilimia 70.
"Pia
katika Mkoa wa Kigoma tuna eneo la Kagunga ambalo kwa sasa hili ni eneo la
kipekee kwa sababu pale TPA imefanya utekelezaji wa miradi mitatu kwenye eneo
moja.Hii ni bahati kubwa kwa Kigoma Vijijini kupata mradi wa namna hiyo na pale
Serikali kupitia Mamlaka imewekeza karibu Sh.bilioni 4. 09, unazungumzia mradi
wa Soko la Kagunga la Sh.milioni 190, mradi wa barabara wa mita 700 wa Sh.milioni
553, mradi wa gati la Kagunga wa Sh bilioni.5. 357,"amesema.
Ameongeza
kuwa kutokana na uwepo wa mradi huo wananchi
wanatakiwa kufahamu pale kuna soko la kimataifa ambalo limelenga kuwaleta
karibu DRC pamoja na Burundi hasa kwa kuzingatia pale ni mpakani mwa Burundi na
Tanzania.Pia kwa maji ni mpaka na DRC,
kwa hiyo sasa watu watakusanyika kufanya biashara kwenye eneo hilo.
"Kwa
tafsiri yetu wananchi wa Tanzania na Burundi watafanya biashara ya kuuza mazao
yao na mnajua wenzetu wa DRC wanatumia rasilimali yao fedha kufanyabishara ya
kununua bidhaa kutoka Tanzania lile ni eneo moja wapo ambalo litavutia
wafanyabishara wengi kwenda kufanyabishara kwenye lile eneo.
"Na
ile Bandari ya Kagunga kwa sasa imekamilika kwa asilimia 100, sisi TPA
tumeshaanza kufanyakazi tangu Desemba 12,mwaka 2019, tayari na wafanyakazi wapo
pale.Nataka niwaambie wana Kagunga na Kigoma kwa ujumla kwamba sasa Bandari
yetu ya Kagunga imeanza kufanyakazi,"amesema.
Salama
amewashauri wenye boti za abiria wapite katika bandari hiyo na kwamba watu
kutoka Burundi na DRC nao wapite hapo na hata wa kutoka Zambia pitieni hapo
kwani watapata huduma kwenye gati na
miundombinu mizuri iliyowekezwa na Serikali kupitia TPA na hayo ndio mapinduzi
ya uboreshaji na uwekezaji wa huduma unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano
chini ya Rais Dk.John Magufuli kupitia TPA chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano.
Boti za abiria zikiwa zimeegeshwa katika Bandari ya Kibirizi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma
Mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika ukiendelea katika eneo la Bandari ya Kigoma.
Mmoja
wa wananchi wa Kigoma Mjini akitoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya
Tano na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kutokana na hatua
iliyochukua ya kuboresha miuomdombinu ha bandari ya Kibirizi na hasa
ujenzi wa gati.
Baadhi
ya mizigo ikionekana katika bandari ya Kibirizi mkoani Kigoma ikisubiri
kusafirishwa kutoka bandari hapo kuelekea nchini jirani za Burundi na
DRC.Bandari ya Kibirizi ni moja ya bandari ambayo imetengewa fedha kwa
ajili ya kuboreshwa kwa miundombinu yake.
Baadhi
ya magari yakiwa yamebeba mifuko ya saruji katika Bandari ya Kibirizi
ambayo inasubiri kupakiliwa na kisha kuingizwa kwenye meli ili
kusafirishwa katika nchi jirani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...