Mwanamke alietambuliwa kwa Majina ya Marry Richard Mushi mkazi wa kijiji cha Kilinga Wilayani Arumeru ameuawa kwa kupigwa na shoka leo Tarehe 25/12/2019 majira ya mchana ikisadikiwa na mwanaume aliyekuwa akiishi naye, ambaye amefahamika kwa majina ya Moses Latiaeli Pallangyo almaarufu kama Moses Lebaba anayejishughulisha na nyimbo za injili.

Tukio hili limetoka ikiwa ni wiki tatu tangu marehemu aanze kuishi na mtuhumiwa kama mke na mume ambapo baba wa mtuhumiwa mzee Latiaeli Samson Pallangyo amesema hapakuwa na ugomvi wowote na walitegemea kusherehekea siku ya Krisimasi  vizuri mara baada ya Mary kuwapikia chai na kisha kuendelea na shughuli za kawaida mpaka mauti ilipomfika kwa kupigwa na shoka chumbani kwake.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro ambae alifika katika eneo la tukio muda mchache baada ya tukio, mbali na kutoa pole kwa wananchi wa kijiji cha Kilinga,  amesema tayari vyombo ya usalama vimeanza msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa na kuwataka wananchi kuwa watulivu na kuviachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake na kuwataka wananchi wenye kujua taarifa za alipokimbilia mtuhumiwa wasaidiane na vyombo vya usalama.
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro (aliyevaa fulana) akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Kilinga na kuwapa pole mara baada ya kufika  katika eneo la tukio muda mfupi baada ya tukio hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...