Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Kufuatia hali ya Uwanja wa Sokoine Mbeya kuharibiwa na Tamasha la Muziki lililofanyika Jana, Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Tanzania Prisons na Yanga mchezo huo utapigwa katika Uwanja ww Samora Iringa.
Taarifa hiyo imetoka mapema leo baada ya Bodi ya Ligi kuufungia Uwanja huo wa Sokoine kutokana na nyasi kuharibiwa vibaya.
Bodi ya Ligi iliamua kubadilisha Uwanja ambapo walipendekeza mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kesho ukapigwe kwenye Uwanja wa Ihefu kama mbadala wa Uwanja wa Sokoine.
Timu zote mbili zimefikia makubaliano hayo baada ya kupokea taarifa ya hali isiyoridhisha kiusalama kwenye Uwanja wa Ihefu ambao ulipendekezwa na Bodi ya Ligi kutumika kwa mchezo huo kesho kama Mbadala wa Uwanja wa Sokoine.
Aidha, wamesema kuwa kwa sasa mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Samora Mkoani Iringa hapo kesho.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulikuwa uchezwe kesho kwenye Uwanja wa Sokoine, na leo asubuhi timu wenyeji walifika Uwanjani kwa ajili ya kufanya mazoezi walishindwa kutokana na Uwanja wa Sokione kuwa katika hali mbaya.
Wasanii wa wasafi walifanya tamasha lao jana usiku kwenye Uwanja huo ambapo wamepelekea kuharibika kwa nyasi za kuchezea kutokana na wingi wa watu na pia kuwepo kwa hali ya mvua Mbeya.
Hii ni moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo Timu za Ligi kuu kwa kukosa viwanja vyao binafsi na kupelekea kuahirishwa kwa baadhi ya mechi zao pindi Viwanja hivyo vinapokuwa na shughuli zingine za kijamii
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...