Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa ,Hamphrey Polepole amewataka wanachama wa CCM mkoa wa Arusha kuhakikisha wanachagua viongozi watakaoleta Mabadiliko ndani ya chama hicho na sio vinginevyo,huku akiwataka Wana-CCM kuvunja makundi yaliopo .

Ameyasema hayo jana wakati akizungumza katika mkutano Mkuu maalumu wa uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Arusha baada ya aliyekuwepo Lootha Sanare kuchaguliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro.

Polepole amesema kuwa,ni vizuri wanachama hao wakawachagua viongozi
watakaokuwa wazalendo wa nchi yao na ambao wanakuwa tayari kutetea maslahi ya chama na wananchi wake kwa ujumla.

Aidha amewataka wanachama wa CCM mkoa wa Arusha kuhakikisha Arusha inaendelea kubaki ya kijani,katika kuhakikisha kuwa wanaimarisha Umoja wao kwa kumchagua Mwenyekiti anayefaa atakae vunja makundi na kukijenga chama .

Katibu wa Organization uchaguzi Makao makuu,Silima Pereira amesema
kuwa,Chama hicho ni lazima kishinde kila mahali kwani kina watu wazuri
ambao wataweza kuiongoza CCM na jamii kwa ujumla na kuendelea kuwapatia ushindi .

Amesema kuwa,na endapo kwa bahati mbaya Chama hicho kikishindwa hatutakuwa na Tanzania tuliyoizoea ,hivyo ni wajibu wetu kuchagua viongozi walio bora ambao watatuweka wamoja.

Mwenyekiti wa muda wa kikao hicho ambaye pia ni Mjumbe wa NEC mkoa wa Arusha,Daniel Hawak ,amewataka wajumbe hao kila mmoja kutambua kilichomleta hapa katika kuhakikisha wanachagua kiongozi aliye bora na sio bora kiongozi.

Aidha wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti mkoa wa Arusha wapo watatu ambao ni Zelothe Steven Zelothe ambae ameshinda kwa kupata kura 468 ,Balozi Batilda Buriani ambae amepata kura 339 huku ambaye ni mgombea wa tatu Bakari Msangi amepata kura 42 ambapo wajumbe waliotakiwa katika kikao hicho 905 ,ambapo wajumbe halali waliofika ni 885 wajumbe waliopiga kura 850 kura halali 849 kura zilizoharibika ni moja .

Akiongea Mara baada ya kutangazwa matokeo balozi batilda Buruani
alishukuru kwa kupata kura hizo na aliwasihi wanachama Wa CCM mkoa Wa Arusha kuacha makundi huku akimsisitiza Mwenyekiti mpya Wa chama hicho kuanza Kazi kwa kuvunja makundi yaliopo ndani ya chama huku akimpongeza Rais Magufuli kwa Kazi nzuri anayofanya ya kusimamia chama pamoja na serikali kwa ujumla.

Naye Bakari Msangi Alisema makundi ndio hula chama cha Ccm na makundi
hayaletwi na wanachama Bali ni viongozi wasio na nithamu katika chama hivyo wajitaidi sana kuyavunja makundi na waache kuvuruga chama Bali washikamane ili kukijenga chama kwa pamoja.

Akiongea Mara baada yakutangazwa kuwa Mwenyekiti mpya Wa CCM mkoa Wa Arusha Zelothe Steven Zelothe alisema kuwa jambo la kwanza anaanza nalo ni kuondoa makundi pamoja na makambi yaliopo ndani ya Ccm mkoa Wa Arusha,alitoa masaa 48 kwa makundi yote kuvunjwa, huku akibainisha kuwa CCM bila makundi inawezekana.

Alibainisha kuwa atahakikisha anasimamia ilani ya chama cha mapinduzi na kuitekeleza ,huku akibainisha kuwa hatavunja maadili kwani anapenda haki ,hapendi vitu vya kuchelewa pia anapenda kusikiliza watu hususa ni wale wanyonge .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...