Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema Sh. Bil. 3.399 za kulipa fidia wananchi 1,526 wa Kikombo ili wapisha eneo la Kikombo
linalojengwa Makao Makuu Jeshi, anazo mkononi.
Amesema utekelezaji wa agizo hilo la Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ulianza Novemba 26 Mwaka huu, siku Moja tu baada ya agizo
kutolewa kwake likimtaka ifikapo Leo, Desemba 1 Mwaka huu awe ameanza kulipa fidia hiyo.
Lakini amesema wanufaika wa zoezi hilo hawajaanza kupokea malipo yao, kutokana na taratibu za ulipaji wa fedha za serikali ambao hata hivyo, Kunambi amesema zipo kwenye hatua za mwisho na wale ambao taratibu zitakuwa zimekamilika wataanza kupokea malipo wiki inayoanza kesho.
“Tupo tayari kulipa fidia lakini zipo taratibu ambazo zinakamilishwa ili zoezi lianze, uhakiki wa malipo unafanywa na wizara ya fedha,
nimeambiwa umekamilika na nitakabidhiwa wiki ijayo.
Pia kuna ambao hawakuwa na akaunti benki huku wengine walionazo zikiwa haziko ‘active’ watendaji wa mitaa wanaendelea kuwasaidia
katika kukamilisha hayo na ninahakika wiki ijayo watakaokuwa tayari wataanza kulipwa," Amesema Kunambi.
Kunambi amesema Kikombo ndiyo utakaokuwa mji mpya wa jiji hilo ambalo litakuwa na miji miwili; wa sasa ambao utakuwa mji wa zamani na
huo mpya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...