Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania
kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeketi leo Jijini Mwanza chini ya
Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Mkutano huo
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya
CCM. Kabla ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa wajumbe walifanya ziara
ya kukagua miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa katika Mkoa wa
Mwanza. Wajumbe pia walipata muda wa kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa
Ilani ya CCM kwa kipindi cha Miaka Minne ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maandalizi na maudhui ya
Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 – 2030 sambamba na Ilani ya
Uchaguzi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa kauli moja kupongeza
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) inayo ongozwa na Ndugu
Rais John Pombe Joseph Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ) inayo ongozwa na Ndugu Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji
mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo mafanikio makubwa ya
kimaendeleo yamepatikana.
Halmashauri
Kuu ya Taifa (HKT) imepokea, kujadili na kuridhia kwa kauli moja Taarifa
ya Kamati ya Usalama na Maadili juu ya uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM wa
kuwasamehe wanachama walioomba radhi kwake baada ya kukiri mbele yake
kufanya makosa ya kimaadili yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake
mbele ya umma.
Wanachama hao ni;-
- Ndg. Januari Makamba (Mb)
- Ndg. Nape Nnauye (Mb) na,
- Ndg. William Ngeleja (Mb)
Kikao cha HKT
kimewataka wanachama hao kujirekebisha na kutorudia makosa yao ama
sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa katiba, Kanuni na
taratibu za Chama ikiwamo kufukuzwa uanachama.
Wakati uo huo, Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeazimia kwa kauli moja na kuelekeza kwamba wanachama wafuatao;-
- Abdulrahman Kinana
- Mzee Yusuf Makamba na,
- Benard Membe
Waitwe na
Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ili wajibu tuhuma za kimaadili
zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na
Uongozi.
Awali Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (HKT) imefanya uteuzi wa majina
ya Wagombea wa nafasi za Uongozi katika Chama na Jumuia kama ifuatavyo;-
- Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha
- Ndg. Batilda Salha Buriani
- Ndg. Zelothe Stephen Zelothe
- Ndg. Bakari Rahibu Msangi
- Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa
- Mafanikio Paulo Kinemelo
- Hilary Adelitius Kipingi
- Lucas Felix Lwimbo
- Wagombea wa nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Mtwara
- Petro Mwendo Mwendo
- Mustafa Nguyahamba Mohamed
- Selemani Manufred Sankwa
- Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Dodoma
- Ndg. Damas Mukassa Kasheegu
- Baraka Andrea Mkunda
- Christopher Thomas Mullemwah
- Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani
- Mary Daniel Joseph
- Fredrick Gasper Makachila
- Samaha Seif Said
Licha ya
hamasa kubwa waliyokuwa nayo wajumbe wa HKT kutokana na kazi nzuri ya
Serikali ya CCM, Ndg. Magufuli amesisitiza kazi ya Urais ni ngumu sana
na yeye ataheshimu utamaduni na desturi za CCM, Kanuni, Katiba ya CCM na
Katiba ya Nchi na kwamba CCM ni kiwanda cha kuzalisha viongozi na kwa
utaratibu ambao chama kimejiwekea kitampata mtu bora zaidi atakayepokea
uongozi baada yake.
Nawashukuru
sana viongozi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ya Chama chetu kwa
kuzisimamia vizuri Serikali zetu mbili na hivyo kuwezesha kupatikana
mafanikio makubwa katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM. Tukaendelee
kujenga umoja, kuimarisha ujenzi wa Chama chetu na tunapoelekea katika
chaguzi zinazokuja tukaepuke makundi, na tuendelee kuisimamia Serikali
ikiwamo kukagua miradi ya kimaendeleo katika maeneo yetu, amesema Ndg.
Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...