Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mafundi mizani nchini wametakiwa
kubadilika na kutumia tekonojia za kisasa ambazo zitachagiza ukuaji wa
uchumi.
Akizungumza na waandishi wa Habari
jana jijijini Dar es Salaam kwa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara
(CBE), wanaosoma mizani Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahel, Ally Hazam alisema,
teknolojia inabadilika hivyo ni wakati sasa wa kuendana na mabadiliko ili
tusiachwe nyuma kibiashara.
Alisema wao kama watengenezaji na
watoaji Mafunzo ya mizani wameamua kutumia mizani ya kisiasa ambayo itasaidia
wafanyabiashara na wateja wao kupata bidhaa halisi kwa kiwango wanachohitaji.
"Wakati sasa umefika wa
kutumia mizani sahihi yenye viwango vinavyohitajika ili kukidhi soko la
Afrika Mashariki...naomba wanafunzi mnaosoma somo hili mkawe walimu kwa
wengine kwakuwa mizani hii inatoa haki kwa anayeuza na
anayenunua,"alisema Hazam.
Alisema wanafunzi wanaosoma somo
hilo watachangia Maendeleo ya nchi kwani ni Idara muhimu kwa Maendeleo ya
Taifa.Alisema mizani yao eanayotengeneza
ni ya kisasa kwakuwa mtu anapata anachostahili na Ina alama maalumbya
Serikali hivyo mtu akijaribu kuichezea ili amuibie mteja wake haufanyikazi.
"Tumeingia ubia na CBE kutoa
elimu hii kwa wanafunzi wao tunaamini somo hili litaleta mabadiliko na kutoa
haki kea wafanyabiashara na wateja endapo watatumia mizani ya
kisasa,"alisema Hazam.Alisema wafanyabiashara wengi
wamekuwa na tabia ya kuchezea mizani ya zamani kwa sababu ya teknolojia
iliyotumika hivyo kusababisha wateja kukosa haki yao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
Mafundi Mizani, Mpasi Hassan ambayr hi Mkurugenzi wa Kampuni ya Henecha
Scale alisema, mafunzo hayo ni muhimu kwao hasa nyakati hizi za
mabadiliko ya kiteknolojia.
Alisema wanaamini watejengewa
weledi utakaoleta mabadiliko na ukuaji wa uchumi.Naye, Naibu Kaimu Mkuu wa Chuo
Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaalam, Respius Kasmir, ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Shahada za awali, alisema Chuo kinatakiwa kitoe mafunzo
yanayoendana na matakwa ya walengwa hivyo waliamua kuungana na Sahel kwakuwa
Ni wadau muhimu wa mizani.
Alisema chuo hicho ndio pekee
Afrika Mashariki kinachotoa kozi ya mizani ambapo nchi ya Kenya nayo huwa
wanatoa kozi fupi.
"Ushirikiano na wadau
unachangia kuleta bidhaa zenye ubora ambapo ndani ya miaka mitatu tumepata
mabadilko ya ongezeko la juu la wanafunzi wa somo hilo ambapo kwa sasa ni
asilimia 40 Hadi 50,"alisema Casmir.
Mhadhiri
Msaidizi katika Chuo cha Biashara (CBE) Boniface Mtasingwa akimkabidhi Cheti cha mafunzo ya Mizani Bartholomeo
Kavishe katika hafla iliyofanyika Chuo cha Biashara CBE Jijini Dar es Salaam
Rais wa
Fani ya Mizani katika Chuo cha Biashara (CBE) Nicholaus Kiyuga akionesha mmoja
ya mizani ya kisasa wakati utoaji vyeti
kwa mafundi mizani iliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Picha
ya pamoja kati ya watendaji wa kamapuni
ya Sahel waigizaji na watengenezaji mizani pamoja watendaji wa chuo cha
Biashara (CBE)
Naibu
Kaimu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaalam, Respius Kasmir,
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shahada za awali akizungumza wakati wa upokeaji wa
mafunzo kwa mafundi mizani waliokuwa wakipata mafaunzo hayo katika chuo cha
Biashara Kampasi ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahel, Ally Hazam akizungumza kuhusiana na umuhimu wa mafunzo kwa mafundi mizani kutokana na teknolojia hiyo kubadilika kila siku wakati wa utoaji vyeti kwa mafundi mizani katika Chuo cha Biashara (CBE).
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahel, Ally Hazam akizungumza kuhusiana na umuhimu wa mafunzo kwa mafundi mizani kutokana na teknolojia hiyo kubadilika kila siku wakati wa utoaji vyeti kwa mafundi mizani katika Chuo cha Biashara (CBE).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...