Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kifungo cha miaka miwili gerezani au faini ya shilingi laki tano kwa aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini (TFF) Jamal Malinzi kwa shtaka ya kughushi nyaraka za muhtasari wa kikao cha kamati tendaji ya TFF huku aliyekuwa katibu Mtendaji   Shirikisho hilo Celestine Mwesigwa akikutwa na mashtaka 2 ikiwemo  kughushi nyaraka za muhtasari wa kikao cha kamati tendaji ya TFF na shitaka la kutengeneza nyaraka za uongo ambapo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani au kulipa faini ya shilingi milioni moja.

Akisoma hukumu hiyo kwa masaa matano Hakimu Mkazi Maira Kasonde amesema kuwa washtakiwa wote walikutwa na mashtaka 30 na mahakama imeona hawana kesi ya kujibu katika mashtaka 10 yakiwemo matumizi mabaya ya ofisi, kughushi nyaraka, kujipatia Fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa Fedha.

Amesema kuwa katika mashtaka ya kujipatia Fedha kwa njia ya udanganyifu yaliyokuwa yanamkabili Malinzi upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha hilo kwa kushindwa kuleta ripoti za Ukaguzi zilizoonesha kuwa fedha zilizopokelewa zilikuwa halali au vinginevyo.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, Kasonde amesema kuwa mashtaka hayo hayajathibitishwa kwa kuwa fedha alizopokea Malinzi ambazo ni dola za kimarekani 173,335 na shilingi 39,100,000 ni marejesho ya mkopo aliyoikopesha TFF.

Amesema ushahidi hautoshelezi kueleza kuwa Malinzi na Mwesigwa walitumia vibaya madaraka yao kwa kuwa hakuna faida waliyoipata na fedha zilizopokelewa zilikuwa ni marejesho ya mkopo.

Pia mahakama hiyo imewaachia huru aliyekuwa mhasibu wa Shirikisho la mpira nchini (TFF)  Nsiande Mwanga na karani wa Shirikisho hilo Frola Lauya.

Awali Wakili wa Serikali Mwandamizi Simon Wankyo aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa adhabu Kali wa washtakiwa wawili ambao ni aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini  (TFF) Jamal Malinzi na aliyekuwa katibu mtendaji wa shirikisho hilo Celestine Mwesigwa.

Wakili wa utetezi Nehemia Nkonko aliiomba Mahakama hiyo kuwapunguzia adhabu  kwa kuwa wamekaa gerezani kwa miaka miwili na nusu, pia washtakiwa hao hawajawahi kukutwa na shtaka lolote hivyo adhabu itakayotolewa izingatie kuwa washtakiwa walitenda hivyo kwa kuiokoa TFF na sio kwa kujinufaisha wao wenyewe.

Nkonko alisema kuwa mshtakiwa Malinzi  amekuwa akisumbuliwa na tatizo la presha na umri wake wake  kwa sasa ni miaka 60, na kwa upande wa mshtakiwa wa pili Celestine Mwesigwa ana mama wa miaka 89 ambaye ni mgonjwa na watoto wadogo ambao wanamtegemea hivyo mahakama iwapatie unafuu wa adhabu.

  Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi pamoja na katibu Mtendaji  wa  Shirikisho hilo Celestine Mwesigwa wakiwa katika chumba cha  Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jioni ya leo mara baada ya hukumu yao kutolewa ya kwenda jela miaka miwili ama kulipa faini ya shilingi laki 500,000/=.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)
 Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi pamoja na katibu Mtendaji  wa  Shirikisho hilo Celestine Mwesigwa wakiwa katika chumba cha  Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jioni ya leo walipokuwa wakisubiri kusomewa hukumu.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)
 Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi pamoja na aliyekuwa karani wa Shirikisho hilo Frola Lauya wakiwa katika chumba cha  Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jioni ya leo walipokuwa wakisubiri kusomewa hukumu.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...