Na Grace Gurisha
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania, leo Desemba 12,2019 imezindua Chama cha Mawakala Tanzania kwa lengo la kuwaweka pamoja ili wajue majukumu yao na majibu wao katika kuendeleza sekta ya bima Tanzania.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na Kamishna wa mamlaka hiyo, Dkt. Mussa Juma baada ya kufanya uzinduzi wa Chama hicho katika ukumbi wa Karimjee, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kufikia uchumi wa kati ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Dkt.Juma alisema bima zinauzwa na Kampuni za Bima , lakini madalali na mawakala wanamchango mkubwa katika kuhakikisha bima inawafikia watu wengi.
"Kwa mantiki hii nchi nyingi ambazo zinamaendeleo makubwa ya bima, mawakala ndiyo wamekuwa na mchango mkubwa katika kukuwa kwa hii sekta. Inamaana uendelezaji wa soko la bima utakuwa umekuwa kwa kiasi kikubwa," alisema Dkt.Juma
Alisema kupitia Chama hicho mawakala hao watakuwa na ufanisi mkubwa kukinganisha na pale ambapo hawana Chama ambacho kinawaunganisha pamoja.
"Kwa hiyo Chama hichi kitasaidia hawa mawakala kuweza kuendeleza sekta ya bima Tanzania kwa sababu tunaamini wao wanaweza kuwafikia watu mbalimbali hadi huko vijijini, " alisema
Kamishna huyo alisema, wanaamini kuwa katika shughuli wanayoifanya watu na Serikali, bima ipo pale kwa ajili ya kuleta ulinzi, ambapo mali zitakapoharibika basi yule mtu anaweza kurudishiwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama hicho, Sayi Daudi alisema walikuwa hawana mahala pa kusemea ,lakini kwa sasa angalau wamepata jukwaa la kuzungumzia masuala yao pia na kitawasaidia kupanga mipango yao.
"Kwa bahati mbaya sana, karibu kipindi cha miaka 18 sekta yetu ya bima haikuwa na chama, kwa hiyo mawakala tulikuwepo tu hatua mahala pa kuzungumzia, lakini hivi sasa mambo yatabadilika kutokana na hichi Chama," alisema Saudi
Naye, Katibu wa chama hicho, Ester Mwamafupa alisema bina inasaidia katika kila eneo, hata bidhaa zinazosafi rishwa kwenda sokoni zinapopata majanga kwa kuharibika au kupotea bima inafanyakazi yake ya kufidia, kwa hiyo wawekezaji wanakuwa na imani zaidi kuwa biashara yao ipo salama.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...