NA ANDREW CHALE, BUSEGA.

MATEMBEZI  maalum ya Baiskeri kutembelea vivutio vya Utalii 'Biking tour'  katika tamasha la Lamadi Utalii Festival,  yameweza kuvutia wananchi mbalimbali mjini hapa huku yakitarajiwa kuwa endelevu.

Wakizungumza muda mfupi baada ya kufika kwenye geti la Ndabaka la kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambapo waliweza kuendesha kwa umbari wa kilometa (KM) 15 toka shule ya Itongo mjini Lamadi mpaka geti la Ndabaka,

baadhi ya washiriki wamepongeza waandaaji wa tamasha hilo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Busega, Bi. Tano Mwera kwa kwa kufanikisha hilo.

"Kutembelea vivutio kwa usafiri baiskeri ni mzuri na unasaidia kuimarisha afya ya mwili na akili.

Tumeona maeneo mengi ya kuvutia na kuimalisha miili yetu. Tunaomba yawe endelevu ili watu wengi zaidi washiriki" alisema mmoja wa washiriki Bwana. Justine Mwelemba.

Katika matembezi hayo  ilishirikisha  watu kumi na  mbili (12) na msafara kupita njia ya (route) ya Lamadi hadi kijiji cha  Nyatwali na kuingia sehemu za vivutio ikiwemo Ndabaka gate ilipo hifadhi hiyo ya Serengeti na baadae waliweza kupitia pori la akiba la kijereshi (Kijereshi game reserve).

Baadhi ya washiriki wa matembezi hayo ni pamoja na maafisa mbalimbali wakiwemo Afisa masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Kanda ya Ziwa  Bi. Rhoda Michel, TANAPA, Chief Warder toka Kijereshi game reserve na Mratibu wa Utalii wa Utamaduni, Nelson Machibya pamoja na wananchi wengine wakiwemo wa Lamadi.

Aidha, Mkuu wa Wilaya  ya Busega ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya tamasha hilo, alisema kuwa kwa sasa wanaangalia namna ya kuboresha utaratibu wa matembezi ya Baiskeri  katika kutembelea vivutio vya utalii lakini pia hata kuhamasisha katika nyanja za kimichezo na afya.

"Huu ni mwanzo. Tunataka matembezi haya ya baiskeri yawe kichocheo. Kwani wageni watakapoona aina hii wananchi watapata ajira ya kutembeza wageni kwenda kwenye vivutio na sehemu zingine zenye huitaji. Lakini pia mbali kuwa zinajenga miili yetu kiafya, tunaangalia kuweka hata mashindano ya mbio za baiskeri ilikuongeza hamasa zaidi" alisema Mkuu wa Wilaya,  Bi. Tano Mwera.

Tamasha hilo kwa mwaka huu ni la kwanza kufanyika, linabena kauli mbiu "Utalii wa ndani unawezekana" limedhaminiwa na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...