Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Richard Kayombo (katikati aliyevaa miwani) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa kodi wa mamlaka hiyo
baada ya kupanga mikakati ya Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi kwa wafanyabiashara
wa eneo la Mabwepande Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inayoendelea
katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam itamalizika tarehe 14 Desemba,
2019.

Mfanyabiashara wa duka la rejareja
wa eneo la Mabwepande Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,
Cathbert Kagirwa akitoa maoni yake kwa Afisa Kodi Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Rose Mahendeka wakati wa Kampeni ya Elimu kwa
Mlipakodi inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam
ambayo itamalizika tarehe 14 Desemba, 2019.

Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Isihaka Shariff akitoa elimu ya kodi
kwa mmoja wa wafanyabiashara wa Kariakoo Wilaya ya Ilala wakati wa
Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea katika maeneo mbalimbali
mkoani Dar es Salaam ambayo itamalizika tarehe 14 Desemba, 2019.

Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Catherine Mwakilagala akitoa elimu ya
kodi kwa baadhi ya wafanyabiashara wa eneo la Tandika Wilaya ya Temeke
wakati wa Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea katika maeneo
mbalimbali mkoani Dar es Salaam ambayo itamalizika tarehe 14 Desemba,
2019.

Afisa
Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zakeo Kowero
akitoa elimu ya kodi kwa mmoja wa wafanyabiashara wa eneo la Kivule
Wilaya ya Ilala wakati wa Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea
katika maeneo mbalimbali mkoani Dar es Salaam ambayo itamalizika tarehe
14 Desemba, 2019. (PICHA ZOTE NA TRA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...