Na, Editha Edward -Tabora
Wakala
wa Barabara za vijijini na mjini TARURA wilayani Igunga Mkoani Tabora
wanatarajia kutumia kiasi cha shilingi Milioni 455 kutengeneza Barabara 2
za kiwango cha lami mjini Igunga yenye urefu wa km 1.3 kwa mwaka wa
fedha 2019/2020
Hayo
yamesemwa na meneja wa TARURA wilayani humo Mhandisi Sadick Karume
katika kikao cha baraza la madiwani wa halmshauri ya wilaya huyo
Karume
ametaja Barabara zitakazotengenezwa ni Igunga-mbutu yenye urefu wa
km1.0 itakayogharimu kiasi cha shilingi Milioni 380 na ile ya CCM
-SingidaRoad yenye urefu wa km 0.3(mita 300)ambapo itagharimu kiasi cha
pesa shilingi Milioni sabini na tano
Pia
amesema ujenzi wa Barabara hizo ni sehemu ya mkakati a wakala huyo
kuboresha Barabara zote za mji huo ikiwemo kuzifanyia matengenezo
makubwa Barabara mbovu zote zinazounganisha vijiji na kata zote wilayani
humo
Aidha amesema
matengenezo hayo pia yataambatana na ujenzi wa mifereji makaravati na
madaraja ili barabara hizo ziweze kupitika wakati wote Huku akibainisha
mchakato wa kuanza ujenzi wa Barabara ya mbutu- isakamaliwa tayari
umekamilika
Wakichangia
hoja baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji miradi ya TARURA
baadhi ya madiwani wamelalamikia barabara za Kata zao ambazo hazipitiki
kutoingizwa katika mpango wa matengenezo kwa mwaka ujao wa fedha
Nao
baadhi ya madiwani waloochangia hoja ni Elisha Anthony wa Kata ya
kining'inila) Jilala Mipawa Kata ya humba na mwenyekiti wa halmashauri
hiyo Lucas Bugota wameeleza kuwa barabara nyingi za vijijini
zinatengenezwa kwa kiwango cha chin sana kiasi kwamba hazikawii
kuharibika hivyo wameishauri TARURA kuobgezewa bajeti ili iweze
kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuwataka wataalamu wa TARURA
kutumia utaalamu wao ili barabara zinazojengwa ziweze kudumu tofauti na
hali ilivyosasa
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Peter Onesmo ambae pia ni
diwani wa Kata ya choma amemtaka meneja wa TARURA wilayani humo kufanyia
kazi ushauri anaopewa na madiwani ili kuepusha malalamiko ya mara kwa
mara kutoka kwa wananchi.
(Katikati)
ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Igunga Peter Onesmo wa
(kwanza kushoto)ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Igunga Lucas
Bugota (wa kwanza kulia ) ni mkurugenzi wa halmashauri hiyo Revocatus
Kuuli wakiwa katika baraza la madiwani mjini Igunga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...