Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imesema itaendelea kupiga vita vitendo vya rushwa, uzembe, ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za umma na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu kwa lengo la kuimarisha uzingatiwaji wa misingi ya maadili, uwajibikaji na utawala bora nchini.
Pia imesema itaendelea na jitihada za kuhakikisha watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla wanapata uelewa kuhusu maadili, haki za binadamu, utawala bora na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa kwa ajili ya kukuza maendeleo.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe George Mkuchika wakati akizungumzia maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu jijini Dodoma leo.
Mhe Mkuchika amesema maadhimisho hayo yataisaidia serikali kuendelea kuthamini namna wanavyoziimarisha Taasisi zao zinazosimamia maadili, haki za binadamu na utawala bora ili kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Amesema utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zinazoshirikiana kuadhimisha maadhimisho hayo ni muhimu katika kulinda na kuhakikisha rasimali za Nchi zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote na wala siyo mtu binafsi au kikundi kidogo cha watu.
" Ni vema jamii yetu ikatambua kuwa uadilifu huanzia ngazi ya familia ndipo serikali itapata watumishi waadilifu wanaozingatia misingi na kanuni za utumishi wa umma, mtumishi mwadilifu atazingatia haki za binadamu anapokua akitoa huduma na hivyo kupunguza kero zitolewazo na wananchi dhidi ya watumishi wetu.
Hivyo tunavyoadhimisha siku ya maadili na haki za binadamu tunatumia fursa hii kujitathimini kama Nchi namna tunavyozingatia maadili, tunavyodhibiti rushwa na pia tunavyofuata taratibu katika manunuzi yetu," Amesema Mhe Mkuchika.
Amesema namna ambavyo serikali inapambana kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kusimamia nidhamu maofisini na kuzingatia misingi ya utawala bora kwa ujumla kunakuza maadili nchini na kuongeza kiwango cha kuzingatiwa kwa haki za binadamu.
" Kusimamia utawala bora na haki za binadamu kumechangia kwa kiasi kikubwa kuondoa ile dhana iliyokuepo kwa baadhi ya viongozi wetu ya kutumia mamlaka waliyopewa kuweka watu ndani, tumekua tukitoa semina kwao na kwa kweli tumefanikiwa sana kuondoa hiyo hali," Amesema Waziri Mkuchika.
Maadhimisho hayo Kitaifa yatafanyika Desemba 10 katika ukumbi wa Pius Msekwa jijini Dodoma na yameratibiwa na na Taasisi zinazoshughulika na masuala ya haki za binadamu na utawala bora, kupambana na rushwa, uwajibikaji, usimamizi wa sheria ba maadili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Kapteni George Mkuchika akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusiana na maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yatakayofanyika Desemba 10 mwaka huu.
Baadhi
ya Wakuu wa Taasisi zinazoshughulika na masuala ya haki za binadamu,
utawala bora, uwajibikaji, usimamizi wa sheria na maadili wakimsikiliza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
bora, Mhe Kepteni George Mkuchika alipokua akizungumzia maadhimisho ya
siku ya maadili na haki za binadamu jijini Dodoma leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...