Anaandika Abdullatif Yunus  Wa Michuzi TV.

Mtanzania Mzalendo aitwae Hussein Salum, kutoka Shirika la kukuza Vipaji na Michezo Shuleni liitwalo Jambo Bukoba, amepata fursa ya  kushiriki kwenye Mkutano wa Dunia wa Vijana Nchini Misri, maarufu kama WORLD YOUTH FORUM akiwa amebeba baadhi ya Vipeperushi kutoka Nyumbani vya "Tanzania Unforgettable".

Baada ya Kufika Nchini Misri Mtanzania huyo pamoja na Watanzania Vijana wenzake, akapanga na kukutana na Watanzania wengine wanaoishi huko kisha kukaa nao mahali na  kuwasimulia mazuri yaliyofanywa na Jembe letu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Kwa kipindi cha miaka minne ya Uongozi wake. Katika hali isiyotarajiwa  wakajikuta wanaanza kuimba mazuri ya Nchi yetu kwa kuimba wimbo wa "Tanzania Tanzania" na ule Wa "Hakuna Matata"  huku wakitaja vivutio vinavyopatikana Nchini.

Hali hiyo imesababisha taharuki Mitaani baada ya vipande vya  Video hiyo, vilipoanza kuruka katika Vituo mbalimbali vya Runinga na Mitandao ya Kijamii Nchini Misri,  hali iliyoongeza morali na shauku kubwa Kwa Raia wa Kigeni kutaka kutembelea Nchini kujionea maajabu hayo, wakiamini kuwa sasa kweli Tanzania Hakuna Matata.

Tayari Mkutano huo  Ulioanza Tarehe 14 Desemba na Kumalizika 17 Desemba 2019, na kukutanisha Vijana kutoka kila pembe ya Dunia, kujjadili masuala mbalimbali yahusuyo Vijana wa Kiafrika hususani Tanzania, juu ya kufikisha ujumbe wa amani, maelewano na ustawi ulimwenguni kote, ikiwa ni pamoja na kuwakutanisha na Viongozi na watu Mashuhuri kujadili masuala ya Amani kutoka katika Nchi zao.

 Pichani Picha ya pamoja ya Vijana wa Watanzania waliowakilisha katika Mkutano wa World Youth Forum uliofanyika Nchini Misri.
 Baadhi ya Vijana washiriki wa Kongamano la Vijana la Dunia "World Youth Forum" wakionesha hati zao za kusafiria kuwakiilisha Nchi zao katika mkutano uliofanyika hivi karibuni Nchini Misri.
 Mtanzania Hussein Salum kutoka Shirika la Jambo Bukoba ambae ameongoza Watanzania wenzake kuyatangaza Mazuri ya Nchi huko Nchini Misri katika Kongamano la Vijana la Dunia lililofanyika hivi karibuni.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...