Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Arusha zimesababisha kukatika kwa mawasiliano katika vijiji vilivyopo kata ya loksale na wilayani Monduli mkoani arusha hali iliyopelekea baadhi ya vifaa vya ujenzi wamabweni ya shule ya sekondari ya loksale kutofika kwa wakati kutokana na kukatika kwa barabara ambazo zinaunganisha kata ya hiyo ya loksale na makao makuu ya wilaya hiyo.

Ambapo hali hiyo imesababisha kukwamisha jitihada za kukamilisha kwa wakati mabweni ya shule ya sekondari Loksale ambapo walitakiwa kukamilisha majengo ya shule mpaka kufikia desemba 15 na waziri wa Tamisemi Suleimani Jaffo kutokana na ongezeko la wanafunzi wadarasa la saba kufaulu kwa mwaka huu 2019.

Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki hii na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Monduli ambae ni Mkuu wa Wilaya hiyo IDD Hassan Kimanta akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kutahmini kuangalia athari ya mvua iliyotokea ya kutembelea baadhi ya maeneo ambayo mvua imeathiri katika kata ya Loksale iliyoko wiLayan Monduli mkoani Arusha.

Hata hivyo amesema kuwa na kuelezea na kubainisha jitihada zinazoendelea kufanyika ikiwemo za kuweka vifusi katika baadhi ya maeneo ili kuunganisha mawasiliano wakati jitihada nyingine zikifanyika.

Amesema kuwa mvua hizo zinzoendelea kunyesha mkoani hapa zimeleta uharibifu mkubwa sana ikiwemo kukatika kwa Miundombinu ya Barabara, ambayo ndio kiungo kikuu cha Mawasiliano katika kata hiyo na makao makuu ya wilay hiyo ya loksale na maeneo ya mjini Arusha.

Kwa upande wake kaimu meneja wa Tarura kutoka halmashauri ya Monduli alisema kuwa Mhandisi Janeth Erasto Mhokera amesema kuwa kufatia mvua hizo ambazo zimeleta uharibifu mkubwa kwa kukosekana kwa mawasiliano kama tarura waefanya jitihada za makusudi ii kuweza kurejesha mawasiliano ya vijiji hivyo na pia wakandrasi wako site kuendelea kumarisha barabara zote katika wilaya ili kuweza kukabiliana na hali ya mvua ambazo zinaendelea kunyesha karibia maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Nae mtendaji wa kijiji wa kata ya Loksale bwana Abeli ulomi alisema kuwa kwasasa hli nimbaya sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa ambapo hali hiyo imekwamisha jitihada za ukamilishaji wa majengo ya mabweni kutokana na ubovu wa barabara kuchimbika kwa bararaba nakukatika kwabarabara hizo .

Mpaka sasa wameshindwa kukamilisha ujenzi wa mabweni hayo ambapo walitakiwa kukabidhi majengo hayo desemba 15 ili kuweza kupokea wanafunzi wakidato cha kwanza ambapoo shule zote nnchini zinatakiwa kufunguliwa januari 6 mwaka 2020 lakini kufatia changamoto hiyo wameshindwa kukamilisha lkn jitihada zinafanywa ili kuweza kukamilisha mabweni hayo kabla ya shule kufunguliwa mwakani.

Kwa upande wake mwananchi bi lucy lazier alisema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa zimeleta athari kubwa hali ambayo imekwamisha jitihaza za ukamilishaji wa mabweni ya shule ya sekondari ya loksale ambapo ameiomba Serikali kuweza kufanya jitihaza za makusudi ili kuweza kupitika kwa barabara hizo na kuweza kupitisha malihgali za ujenzi wa shule hizo na pia waanchi waweze kuendelea na shughuli za uzalishaji mali.

Kwa upande wake bwana john lazier alisemakuwa mvua hizo zimekuwa kikwazo kikubwa cha uendelezaji washughuli za kiuchumi katika kata ya loksale ameiomba serikali kuweza kutengeneza barabara hizo kuweza kurejesha mawasiliano ya kata hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...