Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Watanzania, hususani vijana, wametakiwa kujenga utamaduni wa kusomavitabu ili waweze kupata na kuongeza maarifa ili waweze kufikia ndoto zao katika maisha.
Wito huo umetolewa na na mwandishi wa kitabu cha “Talk to God” (Ongea na Mola), Bw. Masija Buchafwe, alipoongea na waandishi wa habariJijini Dar es Salaam jana wakati akitambulisha kitabu hicho.
“Ndani ya vitabu kuna maarifa mengi ambayo ni msaada mkubwa kwa watuwa rika mbali mbali katika kukabiliana na changamoto za maisha za kilasiku, hivyo itakuwa ni jambo muhimu sana kama taifa watu wake wakawa na utamaduni wa kujisomea vitabu.
"Mimi naweza kuzungumzia Tanzania.Kwa maoni yangu toafauti na miaka ya 1950 hadi 1970 Tanzania ya leohaina watu wenye kiu ya kusoma vitabu,’’amesema Bw. Buchafwe.
Amewaomba wazazi na viongozi katika taasisi za elimu kuwatiamoyo nakuwahimiza vijana kusoma vitabu, na kueleza kwamba kwa tabia watuwenye elimu na maarifa ya kisasa ni watu wanasoma sana na watu
wasiosoma wana maarifa kidogo ya kileo.
“Kitabu hiki mbali ya kuangazia mambo ya kiimani lakini piakimeangazia mambo ya biashara, siasa, uchumi na upendo ambayo yamekuwamuhimu katika kuchochea maendeleo ya mtu binafsi na Taifa kwa
ujumla,’’ ameeleza Bw. Buchafwe na kusema kwamba angefurahi kupokeamrejesho wasomaji wa imani zote.
Bw. Buchafwe amesema kuwa imemchukua takribani miaka 16 kuandaa na kupata mchapishaji ambaye ameyaunganisha mashairi na kuwa kitabu cha kurasa 84.
“Haikuwa kazi rahisi kukamilisha kitabu hiki, changamoto zilikuwanyingi lakini nilizitumia katika kujenga maudhui yaliyobora zaidi kwafaida ya wasomaji,’’ amesema.
Bw. Buchafwe ana Shahada ya Uzamili ya Mahusiano kwa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustiono (SAUT). Ametafasiri vitabu viwilikatika lugha ya Kiswahili kutoka lugha ya Kingereza: Think Big na
God Sent a Man.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...