BODI ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA) imeanzaa mkutano  wa mwaka kwa wahasibu na wakaguzi na hiyo ikiwa ni mwendelezo wa mikutano inayofanyika kila mwaka kwa malengo ya kufanya thathimini pamoja na kuweka mipango mkakati ili kutimiza malengo.

Akizungumza katika mkutano huo Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Charles Kichere amesema kuwa kupitia mkutano huo ili kufanikisha malengo ni lazima kubadilisha mawazo na ujuzi utakaoleta matokeo chanya.

" Kupitia mkutano huu ninaamini mtatoka na mawazo,NBAA wamekuwa washirika wazuri katika kuandaa mkutano wa namna hiyo,  Serikali ipo pamoja na wadau wa maendeleo wapo pamoja katika kuyafikia malengo hayo" ameeleza.

Amesema kuwa bado wanahitaji nguvu ya kutosha katika kujenga uchumi imara na amewataka kufanya kazi kwa bidii na uzoefu walionao katika sekta hiyo ya uhasibu.Na ameshauri kutofanya kazi kwa mazoea bali kwa misingi ya taaluma hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya
Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA) CPA  Profesa. Isaya Jairo amesema wanaendelea kuendelea bodi hiyo hasa kwa kuzingatia maadili ya kazi pamaja na malengo katika sekta hiyo;
"Kama ilivyo dira ya Serikali ya sasa ya kujenga uchumi wa viwanda na sisi tunaamini tutafika pale kwa kuendeleza viwanda na kampuni mbalimbali" ameeleza.

Pia amesema kuwa wanashirikia na wadau mbalimbali ambao zaidi ya 2000 ambao wamehudhuria mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Vilevile Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya
Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA) CPA Pius Maneno programu mbalimbali zitakazojadiliwa katika mkutano huo zitaleta matokeo chanya Kama malengo ya mkutano huo ambao umelenga kujenga uzoefu pamoja na kushirikiana na serikali katika kufikia azma za kimaendeleo.

Amesema kuwa malengo ya kufikia uchumi wa viwanda 2025 yanahitaji uwazi na uwajibikaji wa hali ya juu na kupitia mkutano huo ambao umewakutanisha wadau wa sekta binafisi na umma utatua chachu kubwa katika kuelekea uchumi wa viwanda.
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2019 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere alimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Profesa Isaya Jairo akizungumzia mafanikio waliyoyapata pamoja na namna walivyojipanga kusimamia utendaji wa wahasibu na wadhibiti wa hesabu wakati wa mkutano mkuu wa mwaka 2019 ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) na kufanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno akitolea ufafanuzi kuhusu Bodi hiyo inavyofanya kazi zake wakati wa nkutano mkuu wa wahasibu na wakaguzi wa Hesabu wa mwaka 2019 uliofanyika leo hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
 
 Baadhi ya  wa wahasibu na wakaguzi wa Hesabu wakifuatilia mada wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2019 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2019 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...