Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama akisistiza kwa menejimenti ya NSSF, umuhimu wa miradi ya
nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es
Salaam wakati wa ziara yake ya kukagua uboreshaji wa miundombinu wa
nyumba hizo leo tarehe 18, Desemba, 2019.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisistiza kwa menejimenti ya NSSF,
umuhimu wa miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya Kigamboni
Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kukagua uboreshaji wa
miundombinu wa nyumba hizo leo tarehe 18, Desemba, 2019.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akikagua shughuli za uboreshaji
miundombinu katika miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya
Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18, Desemba, 2019.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na vijana wa SUMA JKT wanahusika
na uboreshaji wa miundo mbinu miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika
wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya
kukagua uboreshaji wa miundombinu hiyo leo tarehe 18, Desemba, 2019.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akikagua shughuli za uboreshaji
miundombinu katika miradi ya nyumba za NSSF zilizopo katika wilaya ya
Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18, Desemba, 2019.
*************************************
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameridhishwa na utekelezaji wa maagizo ya
Waziri Mkuu, Mhe. Kassimu Majaliwa aliyoyatoa mwishoni mwa mwezi
Novemba, mwaka huu baada ya kukagua miradi ya nyumba za NSSF zilizopo
katika wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Akiongea mara
baada ya kukagua miradi ya nyumba za NSSF leo Desemba 18, 2019 baada ya
kukagua miradi ya nyumba za NSSF zilizopo wilayani Kigamboni, Jijini Dar
es salaam, Mhe. Mhagama amesema kuwa Mhe. Waziri Mkuu alielekeza
menejimenti ya NSSF Kuharakisha kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo ili
ziweze kutumiwa na watanzania.
Waziri Mkuu
alielekeza menejimenti ya NSSF kuwasiliana na vyuo vikuu na Taasisi za
elimu ya juu na elimu ya kati, Taasisi za Umma ili kuangalia uwezekano
wa wanafunzi wa elimu ya juu na watumishi wa umma pamoja na watanzania
wenye nia ya kutaka kupanga nyumba hizo waweze waweze kupangishwa kwenye
nyumba za hizo 161 zilizoko Tuangoma, 720 zilizoko Mtoni Kijichi.
“Nimefurahishwa
katika taarifa yenu kuwa mmewasiliana na vyuo kadhaa ikiwemo DUCE ambao
wameonesha nia ya kuomba nafasi za wanafunzi 3000, lakini pia DIT
wanahitaji nafasi za wanafunzi 300, tunawasubiri IFM na taasisi nyingine
za elimu ya juu na Umma,kwa kuwa kwa Mradi wa Kijichi unazo nyumba 720
ambazo zinaweza kupangishwa na wananfunzi 7,200 kwa mantiki hii
inaonesha tunao uwezo wa kukidhi mahitaji ya vyuo vikuu ” Amesema
Mhe.Mhagama.
Mhe. Mhagama,
ameongeza kuwa katika kuhakikisha nyumba hizo zinakuwa mkombozi wa
malazi kwa wanafunzi wa vyuo, hivyo ameishauri menejimenti ya NSSF
kuwapa kipaumbele wanafunzi wa kike kwa kuzingatia kuwa takwimu za hivi
karibuni zimebainisha kuwa maabukizi mapya ya virusi vya UKIMWI asilimia
40 ni kwenda kwa vijana ambapo asilimia 80 ya vijana ni watoto wa kike
wa vyuo vikuu, amabapo mojawapo ya kichocheo cha maabukizi hayo ni
kutokana na kutokuwa na malazi salama.
Waziri Mkuu,
alielekeza TARURA kuhakiksha wannatengeneza miundombinu ya barabara
katika miradi ya nyumba za NSSF, ambapo tayari wamekamilisha taratibu za
awali za ujenzi wa barabara hizo na wataalamu wa NSSF tayari
wamehakiki gharama za ujenzi wa barabara hizo ili kuona kama zinaendana
na uhalisia wa ujenzi utakaofanyika kupitia SUMA JKT. Zahanati
“Katika kuboresha
barabara za mitaa za hizi nyumba nimeonakazi inayoendelea na
wameniambia DIT wanafanya kazi yao ya kuweka taa za sola kwenye
barabara za mitaa yote ya nyumba hizi na watafanya kazi kwa wakati kama
tulivyokubaliana” amesema Mhagama.
Aidha, agizo
jingine kwa menejimenti ya NSSF ilikuwa ni kuboresha miundo mbinu ya
Umeme, maji taka na maji safi, ambapo tayari taasisi zinazohusika na
miundo mbinu hiyo ikiwemo TANESCO na DAWASA wamekamilisha taratibu za
awali za utekelezaji na wameahidi kukamilisha shughuli zake kwa wakati
ili nyumba ziweze kutumika.
Waziri Mhagama
amefafanua kuwa agizo lingine ambalo NSSF wamelitekeleza ni Mthamini
Mkuu wa Serikali kutathimini nyumba hizo na kutoa bei halisi ya soko
kwa sasa ili kuwawezesha Watanzania wengi na hasa watumishi wa Umma
kununua na kupanga katika nyumba hizo.
“Nimefurahishwa
na taarifa mliyonipatia kuwa mthamini mkuu wa serikali atakabidhi ripoti
yake leo kwa NSSF na naamini sasa watu wengi ambao wameonesha nia ya
kupanga au kununua tutawapatia huduma kwa kuwa tunalo kundi la
wanafunzi, watumishi wa umma na watu binafsi wenye uwezo wa kununua
nyumba hizo”, Amesisitiza Mhagama.
Pia, Waziri Mkuu
aliagiza Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni kupewa kipaumbele kwa
nyumba 439 za Nungu ambapo Mkuu wa wilaya na viongozi wa Halmashauri ya
wilaya ya Kigamboni walielekezwa kuwasaidia watumishi wa wilaya na
Halmashauri hiyo kuingia mikataba rafiki itakayowawezesha
watumishi hao kupewa kipaumbele katika kununua au kupanga kwenye nyumba
hizo mara ukarabati utakapo kamilika.
“Nimeridhishwa na
utekelezaji wa shughuli za miundo mbinu kwa hapa Nungu na hivyo
menejimenti ya NSSF wasilianane na Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni
kuwa uboreshaji wa majengo unaenda vizuri ili watumishi tunaowalenga
waweze kutumia nyumba hizo, ” Amesema Mhagama.
Pia Mheshimiwa
Mhagama amefurahishwa na hatua ya LATRA kuanza kutekeleza agizo
la kuanzisha njia za mabasi ya daladala kupitia kwenye nyumba za NSSF
Mtoni Kijichi na Dungu ili kuwezesha wapangaji na wananchi watakaonunua
na kupanga nyumba hizo kupata usafiri wa umma, kama ilivyokuwa
imeelekezwa na Mhe. Waziri Mkuu.
Aidha, Mhe.
Waziri pamoja na kuwapongeza NSSF kuanza kutekeleza maagizo hayo, pia
amewataka wazingatie muda uliowekwa wa kukamilisha kazi hiyo, hivyo
amewataka kufanya kazi usiku na mchana kwa kuzingatia ubora wa kazi.
“Zingatieni
uhalisia wa gharama zinazotumika katika ujenzi wa mradi huu ili fedha za
wanachama zitumike vyema kwa kuonekana fedha zimewekezwa kwenye miradi
yenye tija ” Amesema Mhe. mhagama
Mkurugenzi Mkuu
wa NSSF, William Erio, amesema NSSF imeyapokea maelekezo yote
yaliyotolewa na Mhe. Waziri Mhagama na kwamba watafanya kwa weledi na
ubora ili kuhakikisha kwamba majengo yote yanakamilika haraka na kuuzwa
au kupangishwa.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini NSSF, Balozi Ali Idd Siwa amemhakikishia
Mhe. Waziri Kuwa watatoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha kuwa
maagizo aliyoyatoa yanatekelezwa kwa wakati ili kuhakikisha nyumba hizo
zinawanufaisha watanzania.
Miradi ya nyumba
za NSSF, wilayani Kigamboni Jijini Dar es salaam, ipo katika maeneo
ya Tuangoma jumla ya nyumba 161, Dungu nyumba 439 na Mtoni Kijichi
jumla ya nyumba 720.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...