Said Mwishehe-Michuzi TV-Mwanza
MAWAZIRI wakuu wa wastaafu kwa nyakat tofauti katika Serikali za Awamu zilizopita wamepata nafasi ya kutoa salamu za sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa nchi yetu ambapo kwa sehemu kubwa wamehimiza umoja, amani na mshikamano kwa Watanzania.
Rais Magufuli wakati akizungumza na wananchi katika sherehe hizo ambazo zimefanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, alitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wastaafu kutoa neno lolote katika sherehe hizo.
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinga alikuwa wa kwanza kupata nafasi ya kuzungmza ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Watanzania wote kutokana na kusherehekea miaka hiyo 58 ya Uhuru.Pia alitoa shukrani zake kwa Rais Magufuli.
"Ninamshuru Rais kwa kunipa nafasi, tukuahidi tutaendelea kukuunga mkono kwa kazi ambazo unafanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.Niwaombe Watanzania tushikiriene kulinda amani na utulivu wa Taifa letu kama msingi muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu,” amesema.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa yeye amesema amani ni jambo muhimu katika nchi yetu na kwamba anakumbuka hotuba ya Rais Magufuli ya kuhamsisha Watanzania kutunza amani.
"Mwalimu Nyerere aliwahi kutuambia enzi za uhai wake kuwa akija mtu mtu jeuri na fedhuri na kisha akauliza Watanzania mna nini , mjibuni tuna amani. Hivyo msingi huo wa kwamba tuna amani ndio unaomuwezesha Rais wetu Magufuli kufanya kzi zake, anafanya kazi nzuri sana.
"Kama akiachiwa akapiga miaka yake 10 nchi hii itabadilika, itakuwa nchi kubwa na yenye maendeleo makubwa sana.Nawaomba tumuunge mkono, tumsaidie nchi yetu iende mbele, "amesema Lowassa huku akimpongeza Rais Magufuli kwa kumwabia hongera.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Frederick Sumaye amewapongeza Watanzania na wakati huo huo amempongeza Rais Maguful kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kujenga uchumi wa nchi yetu.
Sumaye amesema kuwa uhuru wa kisiasa ambao leo Watanzania wanasherehekea iwe chachu sasa ya kwenda katika uhuru wa kiuchumi na anaamini kwa kazi inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, nchi itapiga hatua.
"Bado tuna tatizo la utegemezi lakini naamini kwa kazi inayofanywa na Serikali hii ya Awamu ya Tano na zingine zote za nyuma tutakuwa sawa kiuchumi,"amesema.
Waziri Mkuu mstaafu John Malecela amempongeza Rais Magufuli na kwamba kazi ya kuleta maendeleo ambayo anaifanya inaonekana kwa vitendo na watu wakitaka ushahidi waende Dodoma wataona jinsi ilivyobadilika na kwamba Serikali inafanya maendeleo kwa kasi kubwa.
"Kwangu mimi ni Mkoa wa Dodoma, ningependa nieleze watu wa Dodoma tunao ushahidi kwa vitendo kuhusu maendeleo ambayo yanafanywa na Serikali yetu chini ya Serikali ya Awamu ya Tano,"amesema Malecela.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe,Edward Lowassa akiwasalimia wananchi katika maadhimisho
ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri
katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehezilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...