Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imewataka waajiri wote nchini kutuma taarifa za Watumishi wa Kada ya Ununuzi na Ugavi juu ya idadi ya watumishi hao, katika Kitengo, idara hiyo, vyeo vyao, hali ya usajili, ukubwa wa manunuzi katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo na utendaji wao ili Bodi hiyo ifanye tathmini ya uwezo na uhitaji wa wataalamu katika tasnia husika.
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Godfred Mbanyi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Da es Salaam.
Mbanyi amesema katika kutekeleza jukumu hilo, mwezi Oktoba, 2019 Bodi hiyo iliandika barua kwa jumla ya Taasisi za Umma 576 kuzitaka kuwasilisha taarifa za watumishi wote wanaofanya kazi za Ununuzi na Ugavi katika taasisi zao.
Amesema hadi sasa jumla ya taasisi 460 zilizoandikiwa barua hiyo, bado hazijaleta taarifa husika. Amesema suala hilo linakwamisha Bodi kutekeleza wajibu wake wa Kisheria katika kupanga, kuelekeza na kuratibu mahitaji ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ili kuishauri Serikali mahitaji ya Wataalamu katika taasisi za Umma.
PSPTB imetoa wito kwa Wakuu wa taasisi na Waajiri nchini kuleta taarifa za watumishi wanaofanya kazi za Ununuzi na Ugavi kabla ya Januari 31, 2020, pia Bodi hiyo imetoa wito kwa Watalaamu wa Ununuzi na Ugavi kufanya kazi kwa weledi, umakini na bila hofu ili kupata thamani ya fedha kwenye manunuzi.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu waajiri wote kutuma taarifa za watumishi wao wa kada ya ununuzi na ugavi kwa bodi hiyo ili iweze kufanya tathmini ya uwezo na uhitaji wa wataalamu katika taasisi husika.
Baadhi ya wafanyazi wa PSBTB wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...