NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKOA
wa Pwani,umepunguza ajali za barabara kwa asilimia 7.3 ,ambapo
mafanikio hayo yametokana na kufanyika operesheni mbalimbali na kutoa
elimu kwa watumiaji wa barabara.
Aidha
mkoa huo,unaendelea na operesheni nyakuanyakua madereva korofi na
wazembe ambayo imeanza mwanzoni mwa mwezi desemba na itakamilika mwezi
januari 2020.
Akizungumzia
malengo na mikakati ya kudhibiti ajali mkoani hapo, mkuu wa kitengo cha
usalama barabarani mkoani Pwani, Mosy Dozero alisema ,kipindi cha nyuma
kutokea ajali moja ama ajali inayosababisha majeruhi na kifo ilikuwa
ni jambo ambalo halipingiki lakini kwasasa inaweza kupita wiki nzima
kusitokee ajali.
Mosy
alieleza kuwa, wamejipanga kukomesha ajali zembe na kuendelea kutoa
elimu kwa watumiaji wa barabara kwani PWANI BILA AJALI YAWEZEKANA.
Nae kamanda wa polisi mkoani humo,(ACP) Wankyo Nyigesa alifafanua, takwimu
zinaonyesha kuwa tumefanya vizuri mwaka 2019 ,ukilinganisha na mwaka
2018 ,ambapo makosa ya ajali zilisababisha vifo mwaka 2018 yaliripotiwa
41 , mwaka huu 2019 ajali zilizosababisha vifo zilikuwa 32":aliweka
bayana Wankyo.
Wankyo
alibainisha, makosa ya ajali zilizosababisha majeruhi kwa mwaka jana
2018 ziliripotiwa 100 mwaka huu ajali ziliripotiwa 64.:
Alitoa wito na kuwataka watumiaji wa vyombo vya moto,magari,pikipiki,bajaji, toyo
na watembea kwa miguu kuendelea kutii sheria za usalama barabarani
kwakuwa atakaekiuka sheria hizo atachukuliwa hatua za kisheria na
kufikishwa mahakamani.
Wakati
huo huo kamanda huyo ,amepiga marufuku kwa mtu yeyote au taasisi ya
serikali kufyatua fataki siku ya mkesha wa mwaka mpya bila kibali cha
Jeshi la polisi.
Wankyo
anasema, ni marufuku kuchoma tairi katika barabara za umma ama mitaani
kwa kufanya hivyo utakuwa umekaribisha Jeshi la polisi kukukamata na
kukupeleka mahakamani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...