Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mwanza
RAIS DK. John Magufuli ametangaza msamaha kwa wafungwa 5, 533 ambao walikuwa wamefungwa hela kwa makosa mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuonesha furaha yake ya kusherehekea miaka 58 ya Uhuru wa nchi yetu.
Akizungumza mbele ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambazo ndiko zimefanyika sherehe za Uhuru kitaifa, Rais Magufugli alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa siku za karibuni alipaa nafasi ya kutembelea gereza la Butimba mkoani Mwanza na kushuhudia idadi kubwa ya wafungwa na mahabusu, hali ambay o kama binadamu ilimuumiza sana.
“Baadhi yenu mtakumbuka miezi michache iliyopita nilitembelea baadhi ya magereza likiwemo gereza ma Butimba, nilishuhudia kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa wafungwa na kwa taarifa niliyopewa hali kama hiyo haiko kwenye gereza hilo tu bali ni kwa magereza yote nchini na mpaka leo tuna wafungwa 17,547 na mahabusu 18,256, hivyo kwa pamoja wanakuwa 35,803 hii ni idadi kubwa,"amesema Rais Magufuli.
Amesema kuwa kwa kuwa hata Mungu anasehe ambao wamemkosea, hivyo naye kwa mujibu wa Katiba ya nchi anayo mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafunwa ambao wametiwa hatiani, hivyo leo Desemba 9 anatoa msamaha kwa wafungwa 5533 na kwamba watolewe gerezani kuanzia kesho.
Amefafanua wafungwa ambao amawasemehe ni wale ambao wamefungwa kati ya kuanzia siku moja hadi mwaka mmoja na wengine ambao wamekutana na msamaha wa Rais ni wafungwa ambao wamefungwa miaka mingi na tayari wameshatumikia sehemu kubwa ya kifungo chao.
"Tunafahamu kuna baadhi ya wafungwa wamefungwa kwa makosa madogo madogo kama kuiba kuku, kumtukana rafiki yake, kujibizana na mpenzi wake au mshikaji wake na wengine kwa kukosa mawakili wa kuwatetea katika kesi zao lakini wengine kwa kushindwa kulipa fani na kuna wengine wamefungwa kwa kuonewa.
“Kama binadamu hali niliyojionea pale Butimba ilinihuzunisha na kunisikitisha sana ilikuwa hali mbaya, hivyo kwa kutambua kuwa hakuna mwanadamu aliyemkamilifu na wote hapa tumeshatubu na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na kwa kutambua wafungwa wengi wanajutia makosa yao na hawako tayari kuyarudia.
"Ninapenda nitumie nafasi hii kwa mujibu wa madaraka niliyopewa ya kusamehe au kufuta adhamu ya mtu aliyetiwa hatiani na mahakama nimeguswa na nimeamua kusamehe jumla ya wafungwa 5,533,” amesema Rais Magufuli.
Aidha ameagiza wafungwa hao ambao amewapa msamaha waondolewe mara moja kuanzia kesho a hatarajii kusikia au kuona wanafanyiwa mizengwe na kwamba orodha ya wafungwa aliwaowasemehe yote anayo na atakabidhi kwa Kamishan Jenerali wa Magereza.

"Idadi
hii ya wafungwa ambao nimetoa msamaha ni kubwa sana na huenda watu
wakashangaa lakini ninayo madaraka ya kisheria ya kutoa msamaha."amesema
Rais Magufuli huku akiutaja Mkoa wa Kagera kuwa ndio wenye idadi kubwa
ya wafungwa waliosamehewa ukifuatiwa na Mkoa wa Morogoro,Dodoma na Dar
es Salaam.
Rais Dkt John Pombe Magufuli alipotembelea Gereza la Butimba jijini Mwanza na kushuhudia mlundikano mkubwa wa wafungwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...